Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitembelea bandari ya Tanga
(TPA) Leo wakati wa ziara ya kushtukiza na kuagiza kupatiwa maelezo ya ununuzi
wa matishali matatu ambayo hayana uwezo badala ya mawili yaliyoidhinishwa na Serikali na
kutaka ndani ya masaa 20 taarifa hiyo iwe imeshafika ofisni kwake.
Majaliwa
ambaye ametua Tanga kwa kushtukiza na kwenda bandari ya Tanga moja kwa
moja kujionea mambo yaendavyo pia alitoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Mwantumu Mahiza pamoja na jeshi la Polisi kuongeza doria katika
mwambao wa Bahari ya Hindi kuzuia mali za magendo pamoja na uingizaji wa
Sukari kutoka nje ambayo imepigwa marufuku.
Alisema
Mwambao wa Bahari ya Hindi upande wa Tanga ni kinara wa uingizaji wa
mali za magendo hivyo kutaka kikomeshwa mara moja shughuli hizo na
kuongeza kikosi kazi ya kupambana na mali za magendo
Injinia wa Mamlaka Bandari Tanzania (TPA), Felex Mafinga, akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa juu ya ununuzi wa matishali matatu ambayo hayana uwezo badala ya mawili yaliyoidhinishwa na Serikali hivyo kuagiza kupatiwa maelezo ndani ya masaa 20 iwe imeshafika ofisini kwake.
EmoticonEmoticon