MASHINDANO YA MAJESHI KUFUNGULIWA KESHO JWTZ WAWASILI SALAMA RWANDA

August 07, 2016
jei1
Mkuu wa Majeshi ya Rwanda (CDS) Jenerali Patrick Nyamvumba (Kushoto)akiongea na Waandishi habari Hawapo Pichani katika Ukumbi wa Uwanja wa Amahoro Juu ya maandalizi ya mashindano ya majeshi  kwa Nchi za Afrika mashariki yanayotarajia kufungulia Kesho(Jumatatu Agosti  8)Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Mandalizi Brigedia Jenerali martin Kemwanga wa JWTZ. .(Picha na Selemani Semunyu).
jei2
Mwenyekiti wa kamati ya Mandalizi ya Mashindano ya 10 ya Majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki Brigedia Jenerali Martin Kemwanga wa JWTZ kifafanua jambo Mbele ya Waandishi wa habari (Hawapo Pichani)Mjini Kigali kuhusu Maandalizi ya mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Rwanda (CDS) Jenerali Patrick Nyamvuba ).(Picha na Selemani Semunyu).
jei3
Baadhi ya Viongozi  na Wachezaji wa Timu za Jeshi wanaoshikiri Michuano ya Kumi ya Majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yanayotaraji kufunguliwa Kesho katika Uwanja Wa Amahoro Mara walipowasili  katika Mji wa KigalI Nchini Rwanda .(Picha na Selemani Semunyu).
…………………………………………………………………………………………………..
Na Selemani Semunyu ,JWTZ
Timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzani limewasili Salama katika Mji wa Kigali Nchini Rwanda kuungana na Wanajeshi wa Nchi Za Afrika Masahariki katika Mashindano ya majeshi kwa nchi hizo yanayotajiwa kufunguliwa Rasmi kesho(Leo).
Kiongozi wa Msafara wa Timu hiyo Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba Alisema muda mfupi baada ya Timu hiyo kuwasili kuwa Timu iko salama na Wameanza mazoezi mepesi kwa Ajili ya Kujiandaa na Michuano hiyo sambamba na kuzoea hali ya hewa.
“Timun yetu iko vizuri kilizhobaki watanzania waendelee kuiombea Timu yetu kwani maombi yao yakichanganyika na jitihada za Timu basi ushindi utapatikana na ni vema Watanzania walioko Rwanda kujitokeza kushangilia Timu zao,Alisema Brigedia Jenerali mwaseba.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba akizungumza Na Waandishi wa Habari alisema Maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa Michezo hiyo huku Timu zikimalizia hatua za Mwisho za Usajili kwa ajili ya Michuano hiyo
Alisema Wanajeshi 500 kutoka katika Majeshi ya Nchi Nne za Tanzania,Rwanda,Uganda, na Kenya wanatarajiwa kushiriiki katika Mashindano ya Kumi  ya Majeshi ya Nchi za Afrika Mashariki huku Burundi ikiwa imeshindwa kushiriki kutokana na hali ilivyo katika Nchi yake.
Jenerali Nyamvumba alisema anamatumani makubwa na mazungumzo yanayoendelea kuhusu Burundi hivyo Matarajio yake yataifikisha Burundi katika Hatua Nzuri na Hivyo kushiriki katika Michezo hiyo ambayo aliita Muhumi kwa Ushirikiano.
“Michezo hii ni Muhimu kwa Ushirikiano wetu kwani hakuna Mshindi mwisho wa mashindano sote tunakuwa washindi kutokan na kufanikisha kuwa pamoja,Urafiki kama kamajeshi yaliyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki,” Alisema Jenerali  Nyamvumba.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania Brigedia Jenerali Martin Kemwanga  amesema kama kamati waliridhia kuwepo kwa Michezo Mitano ambayo ni Mpira wa miguu,Kikapu,Pete,Mikono na Mbio za Nyika

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »