Naibu waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh.luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari hawapo
pichani mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya ukaguzi wa mazingira
jijini Dar Es salaam iliyochukua takribani siku nne.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano
na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akimsikiliza Afisa wa kiwanda cha azam
juisi mara baada kufanya ziara katika kiwanda hicho.
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Amemuagiza Mkurugenzi
Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw. Boniventure
Baya kumuandikia hati ya zuio ya muda wa siku saba mkurugenzi
wa kampuni ya Maji safi na Maji taka jijini DarEs Salaam na Pwani DAWASCO
Mhandisi Cyprian Luhemeja ya Kueleza kwa nini kampuni hiyo imetelekeza
miundombinu yake ya majitaka na kupelekea uchafuzi wa mazingira katika
jiji la Dar Es Salaam.
Akitoa Agizo Hilo Jijini
Dar Es Salaam Mwishoni mwa mwiki wakati wa majumuisho wa ziara yake
ya ukaguzi wa viwanda, mazingira na miundombonu ya DAWASCO na DAWASA,
NAibu Waziri Mpina alisema hati hiyo itamtaka Mkurugenzi huyo wa DAWASCO
kueleza kwa nini kampuni hiyo haitibu maji yatokayo viwandani
huku ikiendelea kupokea fedha toka viwandani na kuachia maji kusambaa
katika makazi ya watu.
Mpina Alisema kuwa DAWASCO
wamekuwa wakipita katika viwanda mbali mbali nchi na kutoza fedha za
uzalishaji maji taka bila kuyapima maji hayo na kuelekeza katika miundo
mbinu mibovu.
Katika ziara hiyo ya
siku nne, Naibu Waziri waziri aligundua kuwa miundombinu mingi ya DAWASCO
iko katika hali mbaya, huku walinzi wa miundo mbinu hiyo wakifanya kazi
katika mazingira hatarishi kwa afya zao kwa kukosa vifaa vya kujikinga
akitolea mfano kituo cha ku pump maji taka cha gymkhana kinachopeleka
maji taka katika bomba kubwa la majitaka baharini.
“Hati hiyo atakayoandikiwa
mkurugenzi wa DAWASCO itamtaka atueleze kwa nini hali ya miundombinu
ipo hivi, kwa nini hawayatibu maji yanayotiririka kwa wananchi huku
wanapokea fedha toka katika viwanda, na kwa nini wanatiririsha maji
taka katika mto msimbazi bila kuyapima.” Alisema
Akitolea Mfano kiwanda
cha SAdoline kinachotengeneza Rangi, alisema kiwanda hicho kimekuwa
kikiwalipa DAWASCO zaidi ya shilingi milioni moja kwa mwezi kwa ajili
ya huduma ya uondoshwaji wa maji taka kupitia miundombinu ya DAWASCO.
Aidha alisema katika
kiwanda cha kutengeneza vinjwaji laini cha AZAM kilichopo vingunguti,
DAWASCO imekuwa ikipokea zaidi ya shilingi milioni tatu kwa mwezi kwa
ajili ya huduma hiyo lakini DAWASCO wamekuwa wakipitisha maji hayo katikati
ya makazi ya watu na kwenda kuyatitirisha katika mto msimbazi jambo
ambalo kisheria ni kosa.
“Hakuna huduma yoyote
ya kutibu maji inayofanywa na DAWASCO huku wamekuwa wakiendela kupokea
pesa katika viwanda, miundombinu yao ni mibivu, mabwawa ya kuhifadhia
maji taka yamekuwa yakitirirsha maji hayo katika makazi ya watu, kiukweli
nahitaji maelezo ya kutosha kutoka DAWASCO.” Alisema Mpina.
Kwa upande wake Mratibu
wa mazingira wa kanda kutoka NEMC Bw. Jaffari Chimgege alisema kuwa
kutokana na ubovu wa miundombinu ya DAWASCO hali ya jiji la Dar Es Salaam
imekuwa chafu.
Alisema kunahitajika
kazi ya ziada kurekebisha miundombinu hiyo kwani hali hii ikiendelea
wananchi watakuwa hatarini kupata magonjwa hivyo ni lazima kazi ya ziada
ifanyike.
“Inatupasa kila mtu
kjutimiza wajibu wake kwa watu wa viwanda,wananchi na DAWASCO kuhakikisha
maji yanayotiririka yanakuwa yamepimwa na kuonyesha kama hayana madhara
yoyote kwa binadamu na sio kuacha maji taka kutirirka katika makazi
ya watu, hii ni hatari tunahatarisha afya za watanznaia.” Alisema
Chimgege.
Nae Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa wa Mji mpya kata ya Mnyamani, bw. Rahim Gassi alisema anaishukuru
serikali kwa kutembelea mataa wake kwani maji taka yamekuwa yakititiririshwa
na kusababisha watu kupata magonjwa.
Alisema Maji taka hayo
yanayotirirshwa katika mto msimbazi ndiyo maji yanayomwagiliwa mambogamboga
na wakulima kasha kuwauzia watuwatu hali ambayo si nzuri ki afya.
EmoticonEmoticon