Mkuu wa Majeshi ya Rwanda (CDS)
Jenerali Patrick Nyamvumba (Kushoto)akiongea na Waandishi habari Hawapo
Pichani katika Ukumbi wa Uwanja wa Amahoro Juu ya maandalizi ya
mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yanayotarajia
kufungulia Kesho(Jumatatu Agosti 8)Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya
Mandalizi Brigedia Jenerali martin Kemwanga wa JWTZ. .(Picha na Selemani
Semunyu).
Mwenyekiti wa kamati ya Mandalizi
ya Mashindano ya 10 ya Majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki Brigedia
Jenerali Martin Kemwanga wa JWTZ kifafanua jambo Mbele ya Waandishi wa
habari (Hawapo Pichani)Mjini Kigali kuhusu Maandalizi ya mashindano hayo
kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Rwanda (CDS) Jenerali Patrick Nyamvuba
).(Picha na Selemani Semunyu).
Baadhi ya Viongozi na Wachezaji
wa Timu za Jeshi wanaoshikiri Michuano ya Kumi ya Majeshi kwa Nchi za
Afrika mashariki yanayotaraji kufunguliwa Kesho katika Uwanja Wa Amahoro
Mara walipowasili katika Mji wa KigalI Nchini Rwanda .(Picha na
Selemani Semunyu).
…………………………………………………………………………………………………..
Na Selemani Semunyu ,JWTZ
Timu ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzani limewasili Salama katika Mji wa Kigali Nchini Rwanda
kuungana na Wanajeshi wa Nchi Za Afrika Masahariki katika Mashindano ya
majeshi kwa nchi hizo yanayotajiwa kufunguliwa Rasmi kesho(Leo).
Kiongozi wa Msafara wa Timu hiyo
Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba Alisema muda mfupi baada ya Timu hiyo
kuwasili kuwa Timu iko salama na Wameanza mazoezi mepesi kwa Ajili ya
Kujiandaa na Michuano hiyo sambamba na kuzoea hali ya hewa.
“Timun yetu iko vizuri
kilizhobaki watanzania waendelee kuiombea Timu yetu kwani maombi yao
yakichanganyika na jitihada za Timu basi ushindi utapatikana na ni vema
Watanzania walioko Rwanda kujitokeza kushangilia Timu zao,Alisema
Brigedia Jenerali mwaseba.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi
wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba akizungumza Na Waandishi wa Habari
alisema Maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa
Michezo hiyo huku Timu zikimalizia hatua za Mwisho za Usajili kwa ajili
ya Michuano hiyo
Alisema Wanajeshi 500 kutoka
katika Majeshi ya Nchi Nne za Tanzania,Rwanda,Uganda, na Kenya
wanatarajiwa kushiriiki katika Mashindano ya Kumi ya Majeshi ya Nchi za
Afrika Mashariki huku Burundi ikiwa imeshindwa kushiriki kutokana na
hali ilivyo katika Nchi yake.
Jenerali Nyamvumba alisema
anamatumani makubwa na mazungumzo yanayoendelea kuhusu Burundi hivyo
Matarajio yake yataifikisha Burundi katika Hatua Nzuri na Hivyo
kushiriki katika Michezo hiyo ambayo aliita Muhumi kwa Ushirikiano.
“Michezo hii ni Muhimu kwa
Ushirikiano wetu kwani hakuna Mshindi mwisho wa mashindano sote tunakuwa
washindi kutokan na kufanikisha kuwa pamoja,Urafiki kama kamajeshi
yaliyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki,” Alisema Jenerali Nyamvumba.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania Brigedia Jenerali Martin Kemwanga
amesema kama kamati waliridhia kuwepo kwa Michezo Mitano ambayo ni Mpira
wa miguu,Kikapu,Pete,Mikono na Mbio za Nyika
EmoticonEmoticon