Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi
(kushoto) akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa na watumishi wa
Wizara hiyo kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na
Utumishi, Said Msambachi (kulia) aliyestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria
tarehe 16 Juni, 2016.
Hafla hiyo ilifanyika juzi tarehe 05 Agosti, 2016 katika ukumbi wa
mikutano wa Selous, Makao Makuu wa Wizara hiyo, Jengo la Mpingo, jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mstaafu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Said Msambachi (kulia) akitoa nasaha zake kwa watumishi wa
Wizara hiyo katika hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na watumishi hao tarehe
05 Agosti, 2016. Aliwaasa watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa
kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu kama chachu ya maendeleo
yao kazini. Aliwataka pia kufanya kazi kwa ushirikiano kujiepusha na
majungu, vitendo vya rushwa na ubaguzi pahala pa kazi. Kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi, Ziana Mlawa (kushoto)
akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi wote kwa ushirikiano walioupata
kutoka kwa Bw. Said Msambachi (kulia) katika kipindi chote cha miaka mitano alichofanya kazi katika Wizara hiyo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Rasilimali Watu, Idara ya Utawala na Utumishi, Aurelia
Matagi, akitoa ufafanuzi wa ratiba na kuongoza utambulisho katika hafla
hiyo.
Mkurugenzi
Mstaafu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Said Msambachi na Mama Msambachi wakikata Keki ya kuagwa
waliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo.
Taswira ya keki hiyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tatu
kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Utawala, Said
Msambachi (wa pili kulia) risiti ya friji (pichani kulia) aliyozawadiwa
na watumishi wa Wizara hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo katika hafla hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara walioshiriki hafla hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara katika hafla hiyo.
Sehemu ya watumishi katika hafla hiyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi
(kushoto) akizungumza na watumishi walihudhuria hafla hiyo.
Picha
ya pamoja kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (wa pili kushoto, msatari wa mbele), Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Said Msambachi (wa tatu kushoto), Mkurugenzi
anayekaimu nafasi yake kwa sasa ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Utawala, Ziana Mlawa (kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Aurelia Matagi na Watumishi wa Wizara walioshiriki hafla hiyo (mstari wa pili na wa tatu nyuma) .
Picha
ya pamoja kati ya Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Utawala na Rasilimali
Watu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Said Msambachi (katikati) na
Mkurugenzi anayekaimu nafasi yake kwa sasa ambaye pia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala, Ziana Mlawa (kulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Aurelia Matagi (kushoto).(Picha na Hamza Temba - WMU)
EmoticonEmoticon