Mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho ya Kilimo na Mifugo ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika kwenye uwanja wa Taso Themi akipata maelezo kwenye banda la kampuni ya Simba Cement |
Meneja Mauzo wa Simba Cement mkoa wa Arusha,Christopher Mgonja(kulia)akimkabidhi mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo,Thomas Mollel kofia na tisheti . |
Bwana Shamba wa kampuni ya mbegu ya Seed Co,Lukinga Miho akizungumzia kampuni hiyo kuanza kuzalisha mbegu za mbogamboga ambazo zina soko kubwa ndani na nje ya nchi. |
Wananchi wakipata maelezo ya kilimo cha Mbogamboga na Matunda kwenye banda la taasisi ya TAHA inayojihusisha na kuhamasisha wakulima kuzalisha kwa wingi kwaajili ya soko la ndani na masoko ya Ulaya . |
Wananchi wakipata elimu ya kilimo kwenye uwanja wa maonesho ya Wakuma na wafugaji Kanda ya Kaskazini uwanja Taso, Themi mkoani Arusha. |
Wajasiriamali hawakua nyuma kwenye banda la Halmashauri ya Jiji la Arusha kuonyesha bidhaa zao kwa wananchi waliotembelea maonesho ya mwaka huu. |
Wanafunzi nao ni sehemu ya wananchi wanaotembelea maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane pamoja na mambo mengine hujifunza mambo mengi yanaendana na masomo yao kwa vitendo. |
Maafisa wa Benki ya NMB mjini Arusha wakitoa huduma kwa wananchi wanaofika kwenye banda lao. |
EmoticonEmoticon