RC MAHIZA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA BANDARI YA TANGA.

January 13, 2016
MKUU WA MKOA WA TANGA,MWANTUMU MAHIZA AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA BANDARI LEO MARA BAADA YA KUITEMBELEA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,ABDULA LUTAVI NA KULIA NI KAIMU MENEJA WA MAMLAKA YA BANDARI MKOANI TANGA,HENRY ARIKA
NA TANGA RAHA BLOG.
IMEELEZWA kuwa agizo la Rais John Magufuli kusitisha safari za nje kwa watendaji wa serikali nchini zimesababisha Bandari ya Tanga kufanyakazi chini ya kiwango na kulazimika kukodi vifaa kwa gharama kubwa nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa bandari ya Tanga Arika wakati mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alipofanya ziara ya siku mmoja kukagua shughuli zinazofanywa na bandari hiyo.
 

Alisema kuwa hatua hiyo ya kusitishwa kwa safari mpaka vibali
imechangia bandari hiyo kupata hasara na kulazimika kukodi Tug ya kupakuwa mizigo kutoka nangani kwenye meli hadi katika pwani ya bandari hiyo.


“Mheshimiwa mkuu wa mkoa japo agizo hilo linafaida kwa serikali lakini tunamuomba Mheshimiwa Rais angalie upya agizo hilo kwani kuna baadhi ya taasisi zinazojiendesha kibiashara zinaathirika na utendaji wake wa kila siku kushuka”alibainisha Kaimu Meneja huyo.


Aliiomba serikali kuangalia namna bora ya kutenganisha taasisi hizo katika utoaji wa vibali kwani kwa hili limesababisha kushindwa kupelekaTug meli ya kukokotea vyombo vya majini yao kwa ajili ya ukarabati nchini Kenya.
 

“Taji tuliyonayo katika bandari ya Tanga ni mmoja pekee na manahoza waliisimamisha kufanyakazi toka mwezi Novemba mwaka jana hivyo tumelazimika kukodi Tug kutoka mjini Mombasa ili kurahisisha utoaji wa mizigo”alisema Arika.

Ambapo aliongeza kuwa hali hiyo situ inakwamisha utendaji kazi bali inachangia hasara kwa Mamlaka kwani hulazimika kutumia gharama kubwa kwaajili ya uwendeshaji kifaa cha kukodisha.
 

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa uwamuzi wa Rais ni kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana kwa haraka na kwa kutumia raslimali kwa uwangalifu.

Alisema kuwa sambamba na hilo ilikuweza kuongeza ufanisi katika
bandari ameahidi kuunda tume itakayokuwa ikishughulika na kutatua kero mbalimbali zinazoikabili bandari hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi .






MKUU WA MKOA WA TANGA,MWANTUMU MAHIZA KULIA AKIJIANDAA KUINGIA KWENYE BOTI KWA AJILI YA KUFANYA ZIARA YA KUZUNGUKA BANDARINI

KAIMU MENEJA WA MAMLAKA YA  BANDARI YA TANGA(TPA)HENRY ARIKA AKIZUNGUMZA WAKATI ZIARA YA MKUU WA MKOA MWANTUMU MAHIZA LEO WA KWANZA KUSHOTO NI MKUU HUYO WA MKOA NA ANAYEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,ABDULLA LUTAVI








Share this

Related Posts

Previous
Next Post »