Kaimu mtendaji mkuu wa wakala wa
ufundi na umeme TEMESA Eng. Prisca Mkama akitoa taarifa ya utendaji wa
kivuko cha Magogoni kwa Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano profesa
Makame mbarawa kushoto na mkurugenzi wa ufundi dkt. William Nshama
kulia akifuatilia.
Mkuu wa kivuko cha magogoni Eng.
Charles Irege akimwonesha Waziri waziri wa ujenzi,uchukuzi na
mawasiliano profesa Makame mbarawa namna ya kufuatilia mapato ya kivuko
cha magogoni kwa njia ya elekroniki.
Mkuu wa kivuko cha Magogoni Eng.
Charles Irege akimwonesha Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano
profesa Makame mbarawa namna ya kukagua tiketi za kielekroniki kabla ya
abiria kuruhusiwa kuingia kwenye kivuko
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
mawasiliano profesa makame mbarawa mwenye suti akizungumza na wasafiri
wa kivuko cha magogoni eneo la kigamboni kabla ya kuanza safari kulia
kwake ni Kaimu mtendaji mkuu wa TEMESA Eng. Prisca Mkama.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano profesa Makame mbarawa mwenye suti akishuka kwenye kivuko
cha mv. kigamboni mara baada ya kukagua shughuli za kivuko hicho.
Abiria wanaotumia kivuko cha Mv. Kigamboni wakielekea kupanda kivuko hicho kutoka magogoni kwenda Kigamboni.
………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mh.Prof. Makame Mbarawa amewataka Wakala wa Ufundi na Umeme
nchini (TEMESA), kufunga mfumo kamili wa elekroniki katika kivuko cha
Magogoni ili kudhibiti mapato yanayopotea kiholela.
Amesema takriban asilimia 20 ya
abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni na Mv Kigamboni wanavuka bila
kulipa nauli hali inayoathiri mapato stahiki ya kivuko hicho.
“Nawapa miezi mitatu muwe
mmefunga mfumo kamili wa kupokea nauli wa elektroniki ambao utadhibiti
ukwepaji wa kulipa nauli ili kuongeza mapato na kufikia shilingi milioni
25 kwa siku,” amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amesema nia ya
wizara yake ni kukusanya mapato stahiki kutoka katika vivuko vyote ili
kuwezesha kununua kivuko vipya na kukarabati vivuko vingine kadri
iwezekanavyo.
Aidha ameagia ufanyike uboreshaji
wa bwalo la kupumzikia abiria upande wa magogoni ili liweze kuhudumia
watu wengi na katika hali nzuri na kuagiza uboreshaji huo kuanza mara
moja.
Amezungumzia umuhumi wa
wafanyakazi wa vivuko vya Magogoni na kigamboni kuwa na lugha nzuri kwa
abiria wao na kuwasaidia wale wenye mahitaji maaalum ili kuboresha
huduma ya usafiri ya vivuko hivyo.
Ameitaka TEMESA kuweka mfumo wa
tiketi za msimu zitakazowezesha wafanyakazi kulipa kwa awamu moja au
mbili kwa mwaka na hivyo kunufaika na punguzo maalum na kuondoa usumbufu
wa kulipa nauli kila siku.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Eng. Prisca Mkama amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mapato ya
kivuko cha Magogoni yataimarika hivi karibuni kufuatia mikakati
madhubuti wanayoifanya katika kuboresha huduma zao hususani eneo la
Kigamboni.
Tariban abiria elfu 60 hutumia
kivuko cha Mv. Magogoni na Mv. Kigamboni kuvuka kwa siku katika harakati
za shughuli za kijamii na kibiashara.
EmoticonEmoticon