Mganga
Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi (kulia), akibonyeza kituvye
Dar es Salaam leo asubuhi, kuashiria uzinduzi wa mfumo wa utoaji vibali
kwa njia ya kielekitroniki (e-portal) ambao utawezesha Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA), kuhudumia wateja wake kwa kutumia mtandao wa
intaneti. Mpango huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa TFDA na Taasisi ya
TradeMark East Africa (TMEA)
……………………………………
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA
ya Chakula na dawa nchini (TFDA), imezindua mfumo mpya wa utoaji vibali
kwa mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama ‘e-portal’.
Mfumo
huo uliogharimu kiasi cha sh. milioni 300 kwa ushirikiano wa taasisi ya
Trademark East Afrika(TMEA) kwa kutoa dola za marekani 250,000 lengo
ikiwa ni kuboresha mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao.
Akizungumza
Dar es Salaam leo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, Dk.Mkuu wa Serikali Muhammad Kambi alisema
mfumo huo uliozinduliwa umekuja wakati muafaka kwani utasaiduia
kuboresha huduma katika sekta ya afya kwa kuongeza uwazi, ukweli na kwa
uharaka zaidi.
“Mfumo
huu uliozinduliwa leo utarahisisha katika kufanya maamuzi ya kudhibiti
katika utoaji wa vibali vya kuingiza bidhaa nchini na kutoa bidhaa nje
ya nchi kwa kuwa wa kuandaa vibali utafupishwa na utaongeza faida katika
mamlaka hiyo,”alisema.
Alisema
mfumo huo utasaidia kuhudumia wateja na katika kusajili na kufuatilia
ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula,dawa, vipodozi na vifaa
tiba sokoni sanjari na kuongeza kiwango cha wateja katika kuzingatia
matakwa ya kisheria.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo alisema mfumo huo mpya
unatumiwa na watu takribani 300 ambao wamethibitisha kuwa hauna
matatizo yeyote kwani lengo la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanapunguza
muda wa wateja wao katika kuomba vibali ikiwa ni pamoja na kupunguza
gharama za huduma hiyo.
“TFDA
inatambua mchango wa TMEA katika kuendeleza mfumo wa e-portal ambao
utarahisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi na uhifadhi wa taarifa za
usajili, uratibu na ufuatiliaji wa taarifa za ubora na usalama wa
vyakula dawa, vipodozi, vifaa tiba nchini,”alisema.
Mkurugenzi
wa TradeMark East Afrika Tawi la Tanzania, Dk. Josephat Kweka alisema
mfumo huo utasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara hasa katika
kuingiza na kutoa bidhaa katika soko la ushindani.
“Portal
inatarajia kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda
wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa kusafirisha bidhaa nje
ya nchi. Tumewawezesha portal hiyo ili kukuza biashara ya kikanda na
ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za jumuia za Afrika Mashariki,”alisema.
Aidha
uzinduzi huo ni hitimisho la maboresho ya mfumo huo ulioanza mwaka 2011
ambapo utawawezesha wafanya biashara kuomba na kupata vibali vyote
muhimu kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika ofisi za mamlaka hiyo.
EmoticonEmoticon