Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete
akiongozana na Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM wakati
alipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere Rais Jakaya
Kikwete akielekea mkoani Ruvuma na Dk. John Pombe Magufuli akitokea
mkoani Mwanza na kufanya mazunguzo mafupi uwanjani hapo kabla ya
kuagana.
Dk. John Pombe Magufuli
ameendelea na kampeni zake mkoani Dar es salaam ambapo amepokelewa na
vyama mbalimbali vya kisiasa kwa kupamba bendera za vyama vyao kufuatia
ujio wa mgombea huyo ambaye alikuwa akiendelea na kampeni zake za
kuwania Ikulu ya Magogoni mikoani kabla ya kurejea jijini Dar es salaam
kuendelea na kampeni hizo ambazo atazifunga rasmi kwenye uwanja wa CCM
Kirumba mkoani Mwanza Oktoba 24 mwaka huu tayari kwa watanzania kumpigia
kura za ndiyo.
Mgombea huyo amefanya mikutano ya
kampeni katika majimbo ya Kigamboni, Mbagala, Temeke, Ubungo na
Kinondoni huku akiwanadi wagombea ubunge na udiwani wa majimbo hayo,
Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika
jumapili Oktoba 25 mwaka huu.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES
SALAAM)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete
akiagana na Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM wakati
alipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere mara baada
ya mazungumza yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete na Dk.
John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM wakati alipokutana
kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete na Dk.
John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM wakitaniana na mpiga
picha wa gazeti la Jambo Leo Bw. Richard Mwaikenda wakati kwenye uwanja
wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea
Urais kupitia CCM akiwahutubia wananchi na kuomba kura za ndiyo kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini
Dar es salaam
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.
Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba
akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Sinza katika jimbo la Ubungo jijini Dar es salaam.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea
Urais kupitia CCM akiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Sinza
jimbo la Ubungo jijini Dar es salaam leo.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea
Urais kupitia CCM akipokelewa kwa shangwe na mapambo ya bendera za vyama
mbalimbali zilizopambwa kuanzia Ubungo mataa mpaka kituo cha mabasi cha
ubungu kufuatia ujio wa mgombea huyo jijini Dar es salaam kwa ajili ya
mikutano ya kampeni.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea
Urais kupitia CCM akiwanadi wagombea ubunge na udiwani jimbo la Mbagala
kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Zakhem Mbagala jijini
Dar es salaam.
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni wa CCM kwenye uwanja wa Zakhem Mbagala.
Mgombea Udiwani kata ya
Kimbangulile Ndugu Said Fella wa kwanza kushoto akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wagombea wenzake.
Makada wa CCM wakifurahia Kampeni kwenye uwanja wa Biafra.
Mbagala Zakhem ikiwa imetema.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Machava Kigamboni leo.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea
Urais kupitia CCM akimkabidhi ilani ya uchaguzi na kumnadi mgombea
ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea
Urais kupitia CCM akiwanadi wagombea ubunge jimbo la Kinondoni Ndugu
Idd Azzan na wagombea wa viti maalum kutoka kushoto na Mama Madabida na
Mama Janet Masaburi.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea
Urais kupitia CCM akimnadi na kumkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea
ubunge Kinondoni Ndugu Idd Azzan.
Kundi la Orijino Komedi likifanya
vitu vyake jukwaani kwenye mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika kwenye
uwanja wa Biafra huku Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM
na viongozi wengine wakiangalia.
EmoticonEmoticon