WADAU MARA WAMHAKIKISHIA AMANI IGP MANGU

October 01, 2015

X1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Mkoa wa Mara wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo jana.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
X2
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Zeletho Stephen wakati walipokutana jana .IGP yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa huo kukagua utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.
X3
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Zeletho Stephen akizungumza katika kikao cha wadau wa amani mkoani Mara.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.
X4
Baadhi ya wadau wakichangia mawazo katika kikao cha wadau wa amani mkoani Mara kilichohudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.
…………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Wadau wa Amani mkoani Mara wamemhakikishia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kuendelea kuitunza amani  na kuimarisha  usalama katika mkoa huo hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.
Waliyasema hayo wakati walipokuwa wakitoa maoni yao wakati wa kikao kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa amani mkoani humo wakiwemo Wanasiasa, Viongozi wa Uchaguzi, Wagombea, Asasi za kiraia, Viongozi wa dini, Wazee wa kimila na Viongozi wa dini mkoani humo.
Walisema mkoa huo umekuwa shwari hasa baada ya kuundwa kwa Kanda maalumu ya kipolisi ya Tarime na rorya hivyo wananchi wote hawana budi kuendeleza juhudi za Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unaenda salama mkoani humo.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ameahidi Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano wa kutosha na kusimamia vyema uchaguzi ili kuhakikisha kila mwananchi anashiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu bila kutishwa na wahalifu.
Alisema Tume ya Uchaguzi imeweka utaratibu mzuri wa kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo hivyo hakuna haja ya wafuasi kukaa nje ya vituo vya kupigia kura kwa kisingizio cha kulinda kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kujenga mazingira ya kuleta vurugu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe,Zeletho Stephen alisema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari hivyo ni jukumu la kila mdau kuhakikisha anashiriki kwa nafasi yake kuimarisha usalama na amani hasa katika kipindi hiki.
IGP Mangu yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mara kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Polisi ambapo pia amekuwa akitumia fursa hiyo kukutana na wadau mbalimbali ili kushauriana jinsi ya kuimarisha amanai na usalama katika maeneo yao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »