Mjumbe
wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba akiwasili
Jimbo la Simanjiro na kupokelewa na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo
Ndg.Ole Sendeka mapema hii leo.
Mwigulu
Nchemba akimnadi Ole Sendeka kwa wananchi wake,Kubwa ni Ujasiri wa Ole
Sendeka kwenye kutetea maslahi ya taifa,Ufuatiliaji wa Miradi ya
maendeleo kama barabara zinazokwenda kujengwa kwa kiwango cha rami
kuunganisha na mikoa inayopakana na Simanjiro.
Ole
Sendeka akizungumza na Wananchi wake wa kata ya Engesbert kuhusu Ilani
ya CCM na maendeleo ya Jimbo la SImanjiro.Kwenye ilani ya Chama cha
Mapinduzi Jimbo la Simanjiro linakwenda kujengwa barabara za Rami Zaidi
ya Tatu za kutoka Arusha,Mererani na Dodoma na ile ya Babati kwenda
Simanjiro.
Mbali
na hilo,Uboreshaji wa Mfumo wa majini na Uchimbaji wa Visima ndio
kipaumbele cha kwanza kwa Ole sendeka kwa Wananchi wa Simanjiro.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Namalulu Jimbo la Simanjiro.
Twende na Magufuli popote alipo.
Wananchi
wa kata ya Namalulu wakionesha Umoja wao kuichagua CCM kwa nafasi za
Udiwani,Ubunge na Urais katika Uchaguzi wa October 25 Mwaka
huu.
Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa kata ya Namalulu.