Rais
wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati,
Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame
itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka
huu jijii Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari
leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga ameishukuru serikali ya
Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa,
vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na
kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.
Lengo la CECAFA ni kuona vilabu
vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa
ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani
Afrika.
Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi
amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF
itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya amani na
usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.
Timu zilizothibtisha kushiriki
michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia
(Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al
Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani
Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA (Uganda).
Wakati huo Katibu Mkuu wa CECAFA,
Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame
itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam
ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.
Mechi ya ufunguzi tarehe 18
Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji
Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na
Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya
Somalia.
Ratiba ya michuano hiyo imeziweka
timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A lina timu za: Yanga
(Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djbiout), KMKM (Zanzibar) na
Khartoum-N (Sudan)
Kundi B: APR (Rwanda), Al Shandy
(Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia), Kundi C: Azam FC
(Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA
(Uganda)
Timu tatu zitakazoshika nafasi ya
juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na
mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika
hatua ya robo fainali.
BENDERA AIPONGEZA TFF
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta,
Joel Bendera ameipongezs TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13), na maandalizi ya timu hiyo
kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini ya
miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.
Bendera amesema hiyo ndiyo njia
sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio pia amepongeza juhudi za Chama cha
Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na waamuzi,
akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani
Manyara.
Aidha aliwaasa makocha kutumia
mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda kuendeleza
vipaji vya wachezaji watakaowafundisha.
Pia Bendera amewahakikishia
wakazi wa Manyara atahakikisha wanaandaa vipaji vitakvyowawezesha kuwa
na timu bora itakayowakilisha mkoa wa Manyara.
ACCREDITATION FOR ALL AFRICAN GAMES:
Shirikisho la Mpira wa Miguu
barani Afrika (CAF) limetangza kufunguliwa kwa maombi ya vitambulilsho
kwa wandishi wa habari kwenye fainali za michezo ya Afrika
zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo- Brazaville.
Waandishi wa habari wanaotajiwa
kwenda kufanya kazi kwenye michuano hiyo wanaombwa kufanya maombi ya
vitambulisho (Accrediatation) kuanzia Juni 29 mpaka Julai 7 mwaka huu.
EmoticonEmoticon