Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na umati wa watu waliokisanyika
katika banda la NHIF juu ya umuhimu wa watu kupima afya zao mara kwa
mara na kuzingatia kanuni bora za maisha ili kuepuka maginjwa
yasiyoambikiza ambayo mengi husababishwa na unene uliokithiri.
Mh.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF kuhusu huduma zinazotolewa na banda la NHIF katika Maonesho
ya Wiki ya Serikali za Mitaa viwanja vya Mashujaa Mtwara.
Msururu wa wananchi wa Mtwara wakisubiri zamu zao kupima afya zao wakati Mzee aliyejitokeza kupima akipatiwa huduma.
……………………………………………………………
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda leo ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) katika maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa viwanja
vya Mashujaa mjini Mtwara na kuhimiza wananchi kuzingatia afya bora ili
kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama Sukari na Shinikizo la damu.
Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu juu
ya huduma zitolewazo katika banda hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF
Bw. Michael Mhando alisema NHIF anaungana na Serikali katika kupambana
na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuhimiza wananchi kupima afya zao na
kuishi mtindo bora wa maisha unaozingatia lishe bora na mazoezi. Alisema
‘Mfuko umejiwekea utaratibu wa kupima afya bure kwa wananchi kila
unaposhiriki maonesho mbalimbali ili kuwajengea wananchi tabia hiyo na
kuonesha umihimu wa suala hilo ili kuepuka madhara makubwa ya afya na
vifo ambavyo vingeweza kuepukika’
Kwa upande wake Meneja wa NHIF
Mtwara Bi. Joyce Sumbwe alisema tangu maonesho hayo yaaenze tarehe 24
Juni watu 1,800 wameshapimwa afya zao na 32% kati yao wamepatikana na
unene uliokithiri ambao ni chanzo kikubwa cha magonjwa hayo.
Wengi wa wananchi waliojitokeza
walionekana kutokujia kuwa wanatembea na shinikizo la damu na
walishauriwa kwenda kituo cha afya ili kuanza matibabu.
Naye Meneja Masoko na Elimu kwa
Umma Bi. Anjela Mziray alitoa wito kwa wananchi kujiunga na NHIF ili
kumudu gharama za matibabu ambazo ziko juu na magonjwa huja bila taarifa
hata wakati ambapo mtu hana fedha mfukoni. Alisema suluhisho ni kwa
wananchi wote kujiunga na Bima ya afya.
EmoticonEmoticon