BREAKING NEWZZZZZ,MWIGULU NCHEMBA ATUA DODOMA,AREJESHA FOMU YA WADHAMINI ILI ATEULIWE KUWANIA URAIS CCM

July 01, 2015

Mgombea Urais ndani ya CCM Mh:Mwigulu Nchemba akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndugu Luhavi  fomu zilizokamilika idadi ya wadhamini kama Utaratibu wa Chama ulivyoagiza mapema hii leo Mjini Dodoma.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi waliofika kumsindikiza wakati wa kurejesha fomu ya Urais CCM-DodomaBaada ya safari ya ndefu ya Kutafuta wadhamini Mikoani,Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mke wake Bi.Neema Mwigulu akiwasili Makao makuu ya CCM Mjini Dodoma kwaajili ya Kurejesha fomu hizo ilikupisha hatua zingine za ndani ya Chama kuendelea.Mwigulu Nchemba akisaini kitabu cha Wagombea Urais ndani ya CCM.Naibu katibu Mkuu CCM Bara Ndug.Luhavi akiwa amekwisha pokea fomu za wadhamini za Mh:Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba akiwa na Mke wake pamoja na Mwenyekiti wa Wilaya ya Iramba Dr.Makala wakati wa kuzungumza na waandishi wa Habari mara baada ya zoezi la Kurejesha fomu kukamilika.Sehemu ya mamia ya Wananchi waliojumuika na Mwigulu Nchemba wakati wa urejeshaji wa Fomu ya kuwania Urais ndani ya Chama cha mapinduzi.Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari,Kubwa amewashukuru Watanzania(Wanaccm) kwa namna walivyojitokeza kumdhamini Mikoa yote Nchini Tanzania.Amewaomba waendelee kumuunga mkono kwenye hii safari yake ya kuwania Urais Nchini Tanzania.Mwigulu Nchemba akilakiwa na wananchi mbalimbali waliofika kumuunga mkono wakati wa tukio lake la Kurudisha Fomu za Urais CCM-Dodoma.Mwigulu Nchemba akiondoka Ofisi za Chama cha Mapinduzi mkoani Dodoma mara baada ya kukabidhi fomu za wadhamini.Wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio la Urudishaji fomu  za Urais alilolifanya Mwigulu Nchemba mapema hii leo Makao Makuu ya CCM-DODOMA.Bi.Neema Ngure Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba katika picha akiwa na ndugu na Jamaa zake na Watanzania walioungana naye wakati wa kurejesha fomu za Urais.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »