WAZIRI
Mkuu Mstafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa,
amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba
25, mwaka huu.
Mh.
Lowassa ambaye alikuwa amesindikizwa na Wenyeviti wa CCM wa mikoa 12
kutoka bara na visiwani, aliwasili makao makuu ya chama hicho mjini
Dodoma majira ya saa 8:30 mchana wa leo Julai 1, 2015, na kupokewa na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi.
Baada
ya kukabidhi fomu hizo, Mh. Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na
kusoma taarifa yake fupi, ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari
potofu kuwa yeye ni mla rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na
ni kiasi gani, za nani na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo
na kwani yeye ni muadilifu na hana shaka na hilo. Alisema, yeye ana
fedha kiasi gani za kuwapa Wana CCM 874,297, waliojitokeza kumdhamini.
"Maneno
hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo autoe
hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo" Alisema Mh. Lowassa.
Alisema yeye anachukia umasikini, na kwamba endapo chama kitamteua na
hatimaye Watanzania kumchagua kuwa Rais wa awamu ya Tano, atahakikisha
anatimiza dhamira yake ya kuwaondolea Watanzania umasikini.
Mh.
Lowassa, ambaye alisindikizwa na Vigogo wa chama hicho akiwemo, Mzee
Kingunge Ngombale Mwiru, na Mzee Pankrans Ndejembi wakiwemo wenyeviti wa
CCM 12 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, amehitimisha zoezi hilo baada
ya kuzunguka mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, na mara zote amekuwa
akipata idadi kubwa ya wana CCM na wananchi waliojitokeza kwenye ofisi
za CCM mahala alikopita, ikiwa ni pamoja na wengine kujipanga barabarani
na kumpungia mikono
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa (katikati) akizipanga vyema fomu zake ili azikabidhi kwa Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi (kushoto), wakati alipofika kwenye
Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015. Mh. Lowassa
amerudisha fomu hizo, baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini
za WanaCCM wa kumdhamini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais
wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015,
ambapo jumla ya WanaCCM 874,297 walimdhamini.Kushoto kwa Mh. Lowassa ni Mkewe, Mama Regina Lowassa.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab
Luhavi fomu za wanaCCM waliomdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa
kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba
25, 2015. Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa, Mama Regina Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi wakionyesha fomu hizo kwa wanahabari wakati wakikabidhiana, kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi wakionyesha fomu hizo kwa wanahabari wakati wakikabidhiana, kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada
ya kurudisha fomu za wanaCCM waliomdhamini ili apare baada ya ziara yake
ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili aweze kuwania
Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa CCM waliomsindikiza Mh. Lowassa.
Mmoja wa Wanasiasa wakongwe nchini, Mzee Pancras Ndejembi akizungumza machache kumuhusu Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa pamoja na uwezo wake kwenye Chama cha Mapinduzi na kutamka kumuunga mkono kwa asilimia 100.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa akiteta jambo na Mkewe, Mama Regina Lowassa.Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM kutoka Zanzibar, Mzee BoraAfya Ame Silima akitoa neno.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisema machache juu ya imani yake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida akisema machache juu ya imani yake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa.
Mwanasiasa Mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwilu akiweka msisitizo wa aliyoyazungumza siku za nyuma kumuhusu Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg.
Hamis Mngeja na Mwenyekiti wa
Wenyeviti wa CCM kutoka Zanzibar, Mzee BoraAfya Ame Silima, wakati
wakitoka kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1,
2015.
Picha ya Pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa CCM kutoka Mikoa 12 waliomsindikiza Mh. Lowassa kurudisha fomu za udhamini.
Wapigapicha wakitafuta taswira.
Wakongwe wakiongozana: Kulia ni Mzee Kingunge Ngombale Mwilu na Mzee Pancras Ndejembi.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa akiwaaga WanaCCM nje ya Makao Makuu ya Chama, Mjini Dodoma leo
Julai 1, 2015.
EmoticonEmoticon