Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akishiriki
katika swala ya magharibi iliyoswalishwa na Sheikh Jamal Mohammed Abeid
kabla ya futari iliyotayarisha kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba
leo katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba,[Picha na Ikulu.]
Waislamu wa Vijiji mbali mbali
katika Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika swala ya jamaa ya Magharibi
katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba kabla ya kushirikikatika futari
iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein kwa wananchi hao leo, [Picha na Ikulu.]
Waislamu na Waislamu wa Vijiji
mbali mbali katika Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika futari
iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba,
[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili
kulia) akiwa na Viongozi katika futari aliyowaandalia wananchi wa Mkoa
wa Kaskazini Pemba iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu ya Wete
Pemba, [Picha na Ikulu.]
Akinamama wa Vijiji tofauti
vya Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika futari iliyotayarishwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali
Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba kwa wananchi
hao, [Picha na Ikulu.]
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid
na Bi Mauwa Daftari wakiwa katika futari iliyofanyika leo katika Ikulu
ya Wete Pemba ambayo imetayarishwa kwa wananchi wa Mkoa wa kaskazini
Pemba, [Picha na Ikulu.]
…………………………………………………………………………………….
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein jana
aliungana pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari
maalum aliyowaandalia, ikiwa ni miongoni mwa utamaduni anaouendeleza wa
kufutari pamoja na wananchi wa Mikoa yote ya Zanzibar kila ufikapo mwezi
mtukufu wa Ramadhani.
Hafla hiyo ya futari ilifanyika
katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Wete na kuhudhuriwa na wananchi pamoja
na viongozi mbali mbali wa Mkoa huo pamoja na baadhi ya viongozi wa
Serikali.
Aidha, Mama Mwanamwema Shein naye aliungana pamoja na akina mama wenzake wa Mkoa huo katika futari hiyo ya pamoja.
Sheikh Majid Mohammed Abeid
kutoka Wete akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wananchi hao
waliofutarishwa na Alhaj Dk. Shein alitoa pongezi na shukurani kwa
mwaliko huo wa Rais.
Katika shukurani hizo Sheikh
Majid alitumia fursa hiyo kutoa pongezi na kwa mafanikio makubwa ya
kimaendeleo yaliofikiwa katika Mkoa wao wa Kaskazini Pemba chini ya
uongozi wa Alhaj Dk. Shein.
Sheikh Majid alisema kuwa katika
uongozi wa Dk. Shein wameshuhudia uimarishwaji na utekelezaaji wa miradi
mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara za kisasa
katika Mkoa huo ambapo kabla ya hapo walikuwa wakipata usumbufu mkubwa
wa usafiri wa barabara katika shughuli zao za kiuchumi na kijamiii.
Alisema kuwa mbali ya
uimarishwaji wa miundombinu ya barabara katika Mkoa wao huo pia, juhudi
kubwa zimefanywa chini ya uongozi wa Alhaj Dk. Shein katika usambazaji
wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbali mbali ya Mkoa huo.
Aidha, Sheikh Majid alitumia
fursa hiyo kueleza mafanikio makubwa yaliopatikana katika kutatua
migogoro kadhaa ya ardhi chini ya uongozi wa Dk. Shein pamoja na
kupongeza mafanikio katika sekta nyengine za maendeleo na hata za
kijamii.
Sambamba na hayo, Sheikh Majid
hakuchelea kutoa pongezi zake kwa niaba ya wananchi hao wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba kwa mafanikio makubwa yaliopatikana katika kuendeleza
amani na utulivu chini ya uongozi wa Dk. Shein huku akisisitiza haja ya
kudumishwa na kuendeleza kwa manufaa ya Wazanzibari wote.
Sheikh Majid alitumia fursa hiyo
kutoa ombi kwa Alhaj Dk. Shein la kujengewa Bandari yao ya Wete hatua
ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika mchakato wa ujenzi
wa Bandari hiyo sambamba na ukarati wa Bandari iliyopo hivi sasa.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
EmoticonEmoticon