Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Fatma Ali akizungumza na wananchi kabla ya
kuzindua mpango wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni
ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata
huduma hizo katika hospitali kubwa,
2. Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Raphael Mwamoto, akitoa
maelezo kuhusu mpango wa Madaktari Bingwa wanaopelekwa mikoani na Mfuko
huo.
Baadhi ya wakazi wa Mtwara wakisubiri huduma za madaktari Bingwa,
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi.
Fatma Ali akiwa katika picha ya pamoja na madaktari Bingwa baada ya
kuzindua rasmi huduma ya madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Mtwara,
…………………………………………………………………………………………….
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
NHIF unaendelea na mpango wake wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa
ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu
kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa.
Mpango huo pia unalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari
walioko katika hospitali za mikoani ambao watafanya kazi pamoja na
madaktari bingwa hao.
Madaktari waliokwenda Mtwara ni pamoja na wagonjwa ya
akinamama,m magonjwa ya ndani, bingwa wa upasuaji na bingwa wa dawa za
usingizi.
Zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku sita.
Akizindua zoezi hilo Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Fatma
Ali amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mtwara kujiunga na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ili kuujengea uwezo zaidi
Mfuko huo kupeleka huduma za kibingwa katika mikoa mingi zaidi.