Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inadhaminiwa na kampuni ya
bia ya Kilimanjaro, leo inaingia kambini katika hoteli ya Tansoma
iliyopo eneo la Gerezani kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania
kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).
Kikosi
kitakachoingia kambini kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya
Cosafa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20
walioanza kambi tangu wiki iliyopita na wachezaji wanaocheza soka la
kulipwa nchini Congo DR.
Taifa
Stars inatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Gymkana na Uwanja wa
Taifa kwa muda siku mbili kabla ya siku ya alhamis kusafiiri kuelekea
Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa
na mchezo dhidi ya Misri.
Wachezaji
wanaotarajiwa kuingia kambini leo ni Deogratias Munish, Mwadini Ali,
Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Aggrey Morris, Salum Mbonde,
Erasto Nyoni, Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram Mgeveke, Juma Liuzio,
Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco, Mrisho Ngasa,
Salum Abubakar, Ibrahim Hajibu, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
Wachezaji
waliopo kambini tangu wiki iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum
Telela, Peter Manyika jr, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein,
Aishi Manula, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Kelvin Friday, Malimi
Busungu, Bennedict Tinoco, Rashid Mandawa, Atupele Green, Haroun
Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel
Michael, Deus Kaseke.
Msafara
wa Taifa Stars unatarajiwa kuondoka nchini Alhamis Juni 4, 2015
kuelekea Ethiopia ukiwa na wachezaji 23,benchi la ufundi pamoja na
viongozi .
Mechi
kati ya Misri dhidi ya Tanzania inatarajiwa kuchezwa Juni 14, 2015
katika uwanja wa Borg El Arab pembeni kidogo ya jiji la Alexandria.
Wakati
huo huo Tanzania imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu
ya Taifa ya Rwanda kati ya Juni 6, 7 mwaka huu jijini Kigali, kwenye
kumbukumbu ya mauaji ya kimbali, Tanzania itapeleka kikosi cha vijana
U23 katika mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa wiki.
Kufuatia
kupata mwaliko huo kikosi cha U23 kitaondoka nchini ijumaa tarehe 5,
Juni 2015 kuelekea nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 18 chini ya kocha
Salum Mayanga.
Kocha
wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime ameongezwa kwenye benchi la ufundi
litakalokwenda Ethiopia kisha nchini Misri kufuatia kocha Salum Mayanga
kuwa na timu ya U23 nchini Rwanda.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
T: +255 22-2861815 I F: +255 22-2861815 I C: +255 713 455970
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania