Waziri wa Habari Utamaduni Utalii
na Michezo Said Ali Mbarouk akisalimiana na Balozi wa Malawi Nchini
Tanzania Hawa O. Ndilowe wakati alipowasili Ofisini kwake kwaajili ya
kujitambulisha pia na kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusuUtalii
Zanzibar.PICHA ZOTE NA MIZA OTHMAN-HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Afisa Ubalozi anaeshughulikia
masuala ya Uchumi Tanzania Chinvano Kapeleta akizungumzia masuala ya
Uchumi na Utalii na Viongoizi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na
Michezo Zanzibar
Waziri wa Habari Utamaduni
Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk katikati akiwa katika picha ya pamoja
na Balozi wa Malawi Hawa O.Ndilowe kulia yake na baadhi ya viongozi
waliofika Ofisini kwake Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii
na Michezo Said Ali Mbarouk akifafanua jambo katika mazungumzo
na Balozi wa Malawi Nchini Tanzania Hawa O. Ndilowe wakati walipokutana
Ofisini kwake Zanzibar.
………………………………………………………………….
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni
Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok amesema ushirikiano katika
Nyanja za utalii,utamaduni na michezo ndio njia pekee ya kukuza
uhusiano uliopo kati ya Nchi ya Zaanzibar na Malawi
Hayo ameyasema huko Wizara ya
Habari Utamaduni ,Utalii na Mchezo wakati alipokutana na Balozi mpya wa
Malawi Nchini Tanzania Bi Hawa O.Ndilowe alipofika ofisini hapo kwa
kujitambulisha kwa waziri huyo.
Amesema ushirikiano huo utafanya
mataifa yao kutembeleana katika Nyanja hizo na kubadilisha mawazo na
kuongeza uhusiano wao unaimarika kwa kukutana mara kwa mara.
“Tumekuwa na mashindano ya Kombe
la Mapinduzi kila mwaka na nchi mbalimbali ambazo zinashiriki ni vyema
Malawi nayo ikashiriki katika kombe hilo na ushirikiano wetu utakuwa
zaidi”alisema Waziri Said.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa
kwa vile Malawi imepiga hatua kimaendeleo katika masuala ya utalii
michezo na Utamaduni itakuwa ni faraja kubwa kushirikiana katika njia
hizo na kuona Zanzibar nayo inasonga mbele katika nyanja hizo.
Waziri Mbarouk amemshukuru
balozi huyo na kumtaka kufanya ziara nyengine ya kuitembelea Zanzibar
pamoja na familia yake kwa kujionea sehemu mbalimbali za vivutio vya
kiutalii na kihistoria.
Nae Balozi Ndilowe amemshukuru
Waziri kwa mapokezi hayo na kusema kuwa ushirikiano wa Malawi na
Zanzibar ni ushirikiano wa muda mrefu,hivyo kushirikiana katika masuala
ya utalii, utamadu na michezo ni kukuza uhusiana wao uliopo.
Amesema atazishawishi nchi
nyengine pamoja na wageni mbalimbali kuja kutembelea Zanzibar katika
Nyanja tofauti kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi na Mataifa yao.
EmoticonEmoticon