RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA NNE WA MABALOZI JIJINI DAR ES SALAAM

May 27, 2015
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani.)
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi  kuwathamini Watanzania waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora. 
Mhe. Rais Kikwete akiteta jambo na Waziri Membe kabla ya kuwahutubia MabaloziWaziri Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Mabalozi Mhe. Rais Kikwete akiongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Balozi Sefue,  Balozi Mulamula, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mhe. Mussa  Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wote.
Mhe. Rais Kikwete na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »