Maafisa
sita wa shirikisho la soka duniani Fifa wamekamatwa katika hoteli moja
mjini Zurich,Switzerland. kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya
rushwa.
Watuhuhumiwa hao ambao wanasemekana kuwa ni pamoja na
makamu wa rais wa Fifa,wanashikiliwa wakisubiri kusafirishwa kwenda
Marekani.
Shutma hizo zinahusisha rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20
Wanachama
wa Fifa wanakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku
ya ijumaa, ambapo rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter anawania muhula
wa tano.
Mwana mfalme Ali Bin Al-Hussein wa Jordan,ambaye ndiye
mpinzani pekee wa Blatter amesema tukio hilo ni "baya kwa maendeleo ya
soka".
Gazeti la New York Times
limesema askari kanzu walichukua funguo za chumba cha hoteli kutoka eneo
la mapokezi ya hoteli ya Baur au Lac hotel ambayo maafisa hao walikuwa
wakiishi na kuingia vyumbani mwao.Gazeti hilo limesema Operesheni hiyo
ilifanyika kwa utulivu.
Jeffrey Webb, Mkuu wa shirikisho la
Amerika ya Kaskazini na Kati na Visiwa vya Caribbean ametajwa kuwa mmoja
kati ya maafisa waliokamatwa.
Maafisa wengine wa Fifa walishuhudiwa na BBC wakisindikizwa na Polisi kutoka kwenye hoteli hiyo ni:
Mkuu
wa Shirikisho la soka la Costa Rica, Erduado Li, ambaye alikuwa
akitarajia kuwepo kwenye mkutano wa kamati ya Fifa siku ya
ijumaa.Wengine ni rais wa shirikisho la Uruguay Eugenio Figueredo,rais
wa shirikisho la soka Amerika kusini Conmebol na wa Brazil,Jose Maria
Marin,mwanakamati ndani ya Fifa,Polisi walionekana wamebeba mikoba yake
kwenye mifuko ya Plastiki.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa
vipi Blatter amekuwa Kiongozi wa Fifa kwa muda mrefu, pamoja na kuwepo
kwa ripoti nyingi za vitendo vya rushwa lakini ameendelea kushikilia
wadhifa huo.
Wizara ya sheria ya Uswiss imesema katika tamko lake
siku ya jumatano kuwa maafisa wa serikali ya Marekani waliwashuku
maafisa hao kupokea rushwa ya dola milioni 100, tangu mwanzoni mwa miaka
ya 1990 kwa ajili ya michuano ya Amerika ya kati.
Serikali ya Uswiss imesema itaidhinisha haraka kusafirishwa kwao.
Mwanzoni
mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu baadhi ya wafanyakazi wenzake
wa zamani walikuwa wakichunguzwa lakini amekanusha kuwa uchunguzi huo
ulimhusu pia.
CHANZO.BBC
CHANZO.BBC
EmoticonEmoticon