Nyalandu anatakiwa kufanya kazi ambayo CCM imempa na si kutafuta watu wa kumtetea

March 19, 2015

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania mstaafu . Jenerari Mrisho  Sarakikya akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea kata ya Sing’isi na kuaslimiana na wananchi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha yenye lengo la Kukagua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi  na kuhamasisha uhai wa chama cha Mapinduzi , Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mbunguni akiwahutubia wananchi katika mkutano huo Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amemshutumu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kwa kutosikiliza ushauri alioutoa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa wilayani Loliondo na Ngorongoro  kwa mawaziri ambao wizara zao zinahusika moja kwa moja katika maamuzi na kushughulikia matatizo ya migogoro ya Ardhi mkoani Arusha ambapo kumekuwa na migogoro karibu wilaya zote, kati ya mbuga za wanyama na vijiji ama kati ya vijiji na vijiji.
Nape amesema wakati waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiitikia na kupokea ushauri huo na kuhamishia shughuli zake mkoani Arusha ambapo kwa sasa yuko mkoani humo akikutana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi ili kutatua migogoro hiyo,  Nyalandu amekaa kimya anaendelea na mambo yake.
CCM ndiyo yenye mkataba na wananchi kwani ndiyo iliyoomba kura kwa wananchi na Mh Waziri Nyalandu ana mkataba na CCM ambayo imempa kazi ya ili atatue matatizo ya wananchi si sawa,  CCM haiwezi kukubali mambo yaiharibike kwa watendaji wa serikali kutowajibika kwa wananchi kwani ndiyo itakayoadhibiwa na wananchi, “Hivyo Nyalandu anatakiwa kufanya kazi ambayo CCM imempa na si kutafuta watu wa kumtetea Nape” Amesema.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MERU-ARUSHA
2 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kati kutoka kwa Nelson Kitomari Katibu wa MC4 Change kanda ya Kaskazini mara baada ya kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika kijiji cha Sing’isi. 12Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee kata ya akeri Meru Amani Ole Silanga akiwahutubia wananchi katika mkutano uliofanyika kijiji cha Sing’isi. 13 
Baadhi ya mashine za kuvuna mpunga kwa ajili ya wakulima wa mpunga USA River Lekitatu 18 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Bi. Husna Mwilima akizungumza na wananchi wakati akielezea mkakati wa serikali ili kutatuo mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Maweni; 20 
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara kata ya Mbuguni. 25 
Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mbuguni. 26 
Bw. Amani Ole Silanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mbuguni Meru. 27 
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo. 28 29 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa Mgorole kama ishara ya  heshima  ya wazee wa Meru.
31 
Nape Nnauye akivishwa mgorole kama ishara ya heshima ya wazee wa Meru

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »