Naibu Waziri wa Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Juma Nkamia akijibu swali la
Mhe.Haroub Shamis Mbunge wa jimbo la Chonga kuhusu jinsi gani serikali
inawasaidia waadishi kuandika habari za kibiashara,Mjini Dodoma.
Mhe.Victor Kawawa akichangia hoja
juu ya Muswada wa sheria ya udhibiti wa Ajira za wageni wa mwaka 2014
uliyosomwa na Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka, leo tarehe
18/03/2015 bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Janet Mbene akijibu swali la Mhe.Philipa Mturano Mbunge wa
viti maalum lililokuwa likihoji ni namna gani Serikali imejipanga
kuthibiti biashara ya vyuma chakavu kutokana na kuwepo na wizi wa
mabomba.
Waziri wa Kazi na Ajira
Mhe.Gaudensia Kabaka akisoma muswada wa sheria ya Udhibiti wa Ajira kwa
Wageni ya mwaka 2014 kwa mara ya pili ndani ya Bunge, leo tarehe
18/03/2015 Mjini,Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya (kushoto) akizungumza naWaziri wa Habari, Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Fenella Mukangara nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kikao, Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya
Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Mhe.January Makamba (kulia)pamoja na
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe(kushoto) wakifurahi pamoja na
Walimu na Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Dar es Salaam Independent
nje ya Bunge mara baada ya kikao cha bunge, leo tarehe 18/03/2015 Mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa TAMISEMI
Mhe.Aggrey Mwanri akijibu swali la Mhe. Dkt Festus Limbu Mbunge wa
Magu,lilikuwa likihoji ni kiasi gani cha kodi ya Majengo kimekusanya
katika kipindi cha miaka mine na nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa
2014/2015.