Mratibu
wa Mradi wa MDOTS unoafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli
(Sickle Cell) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Robert Mongi
(kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania
waliofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa simu 150 aina ya ZTE
zitakazotumiwa na wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video
wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo
kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi
sahihi ya dawa hizo.
Mkuu
wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kulia) akimfungulia boksi
lenye moja ya simu kati ya 150 aina ya ZTE, Mratibu wa Mradi wa MDOTS
unoafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli (Sickle Cell) katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt Robert Mongi wakati wa makadhiano
ya msaada wa simu hizo zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya wagonjwa
wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa
huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa
ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Mkuu
wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kushoto) akimkabidhi
boksi lenye simu 150 aina ya ZTE, Mratibu wa Mradi wa MDOTS unoafanya
utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli (Sickle Cell) katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, Dkt Robert Mongi, Kwa niaba ya wagonjwa wa
sikoseli msaada wa simu hizo zilizotolewa na mfuko (Vodacom Foundation)
kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati
wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila
watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya
dawa hizo.
Mtoto
Nira Khamis (12) anayesumbuliwa na Ugonjwa wa Siko Seli akionesha simu
aina ya ZTE ambayo atatumia kwa ajili ya kujirekodi na kutuma video
wakati wakimeza dawa. Jumla ya simu 150 zimetolewa msaada na Vodacom
Foundation katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa
siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa
huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili
ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo. Wanaoshuhudia
katika picha ni mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma
(kushoto) na Mratibu wa matibabu kwa njia ya teknolojia Dkt .
Deogratius Soka.
Mkuu
wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kushoto)akimkabidhi moja
ya simu kati ya simu 150 aina ya ZTE, Mtoto Nira Khamis(12)
anayesumbuliwa na ugonjwa wa Siko Seli ambayo atatumia kwa ajili ya
kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa. Jumla ya simu 150
zimetolewa msaada na Vodacom Foundation katika hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video
wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo
kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi
sahihi ya dawa hizo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamebeba maboksi yenye simu
aina ya ZTE walipofika kukabidhi msaada wa simu 150 zilizotolewa msaada
na Vodacom Foundation katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya
wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za
ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo
kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamepozi kwa picha kabla ya
kukabidhi msaada wa simu 150 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation
katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli
kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na
kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya
kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
Tatizo la Ugonjwa wa Siko Seli ni kubwa nchini na limekuwa likiongezeka kila mwaka ambapo hadi kufikia sasa watoto wapatao 11,000 nchini wanazaliwa wakiwa na ugonjwa huu hatari ambao husababisha upungufu wa damu mwilini.
Hayo yamebainishwa na Dk Robert Mongi ambaye ni mratibu wa kitengo cha Siko Seli kwa watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati wa kupokea msaada wa simu 150 za mkononi kwa ajili ya kuratibu matibabu ya wagonjwa wanaotibiwa kwenye kitengo hicho zilizotolewa na kampuni ya Vodacom kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation.
Dk. Mongi alisema tatizo la ugonjwa huu ni kubwa na unatibika iwapo mgonjwa atapima na kuanza kutumia madawa mapema ikiwemo kuzingatia masharti anayopaswa kufuata mgonjwa.
Alisema hivi sasa vipimo vya ugonjwa huu vinapatikana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tu ,hali ambayo inasababisha waathirika wa ugonjwa huu wanaoishi nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuchelewa kupata vipimo na wengi wao kupoteza maisha.”Kutokuwepo na mashine za kufanyia kipimo cha ugonjwa huu za kutosha ni moja ya changamoto kubwa inayokwamisha kuutokomeza kwa kuwa kuna idadi kubwa ya wagonjwa sehemu mbalimbali za nchi wanashindwa kufanya vipimo na kuugundua ugonjwa mapema ili waanze kutumia dawa”.Alisema
Aliishukuru Vodacom Foundation kwa msaada huo wa simu ambao alisema utawafikia walengwa ambao ni wagonjwa wanaotumia dawa na zitasaidia kuratibu matibabu yao kwa kupigwa picha wanapokuwa wanameza dawa wakiwa majumbani kwao na picha hizo kuwasilishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kuwekwa kwenye mfumo wa kumbukumbu za matibabu ya wagonjwa.
Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhi msaada huo Meneja wa Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza ambaye aliambatana na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom alisema kampuni ya Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation imeona kuna umuhimu wa kuwapatia wagonjwa simu ili ziwasaidie wakati wa matibabu yao.
“Tunajua kuwa kuna makundi mengi ya wahitaji katika jamii hivyo tumeona safari hii tuangalie kundi la wagonjwa wanaotibiwa Siko Seli kwa kuwa ugonjwa huu unazidi kuongezeka na unahitaji jitihada za ziada kutoka kwa wadau mbalimbali katika kuutokomeza”.Alisema Rwehikiza.
Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ya kuleta mabadiliko kwenye jamii hususan katika sekta ya elimu na Afya bila kusahau makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii.

EmoticonEmoticon