Mkurugenzi
wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),
Harold Sungusia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo asubuhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba, wakati akitoa taarifa juu ya
mwenendo na hatua za kisheria kwa viongozi wa umma wanaokiuka
maadili.Katikati ni Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo na Uwajibikaji wa LHRC,
Imelda Urrio na kulia ni Ofisa Programu Dawati la Waangalizi Watendaji
wa Serikali wa LHRC, Hussein Sengu.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imepoteza sh.bilioni 250 kwa kipindi cha miaka 9 kutokana na matumizi
mabaya ya fedha za umma, ikiwemo rushwa na ubadhilifu wa mali
mbalimbali.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba Dar es Salaam leo
asubuhi wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo na
hatua za kisheria kwa viongozi wa umma wanaokiuka maadili.
“Katika
kisichozidi miaka 9 kumeripotiwa kashfa kubwa nne ambazo kwa ujumla wake
zimeisababishia taifa hasara ya zaidi ya sh. bilioni 250 ambapo kwa
wastani inapoteza takribani asilimia 20 ya bajeti yake ya mwaka” alisema
Sungusia.
Sungusia
alizitaja kashfa hizo kuwa ni pamoja na mabilioni ya shilingi kupitia
ununuzi wa rada iliyotumika kutoka Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza,
wizi wa mabilioni katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) ndani
ya Benki Kuu (BoT), mkataba usio na tija kwa taifa na kampuni ya
Richmond, kashfa ya mabilioni ya pesa waliogaiwa viongozi wa juu kutoka
akaunti ya Tegeta Escrow.
Alisema
licha ya kuwepo vyombo vya kusimamia maadili ya viongozi wa umma
haliminaendelea kuwa mbaya siku hadi siku kwani rushwa inaendelea
kushamiri na matumizi mabaya ya rasirimali za umma na viongozi
wameendelea kujipatia fedha kwa njia zisizo halali.
Sungusia
aliongeza kuwa bado kauli za kejeli na dharau zimeendelea kutolewa na
viongozi wanatuhumiwa na zaidi ya yote hata mapendekezo yaliyowekwa
katika rasimu ya pili ya katiba na Tume ya Kukusanya maoni juu ya
maadili ya viongozi yametolewa.
Alisema
pamoja na kuwepo na Katiba na Sheria yenye muongozo juu ya maadili ndani
ya muongo huu kumekuwepo na matukio makubwa ya ukiukwaji wa maadili kwa
viongozi wa umma ambapo viongozi wetu wamekuwa na matumizi mabaya ta
rasilimali za umma pamoja na kujilimbikizia fedha na mali kinyume cha
sheria.
Aliongeza
kuwa pamoja na angalizo la kikatiba jitihada za Bunge kama muhimili
wenye dhamana ya kusimamia serikali zimekuwa zikikwamishwa na Serikali.
“Mwenendo
wa kuweka pingamizi Mahakama kuu kuzuia baraza la maadili kufanya kazi
yake kikatiba limeonesha mwanya na udhaifu wa sheria na vyombo vya
kusimamia maadili ya viongozi wa umma.
Alisema
kwa kuwa sekretarieti inaundwa kikatiba inakazi, nguvu na mipaka yake
na inatakiwa kutoingiliwa pale inapokuwa inashughulikia masuala ya
kimaadili.
Aliongeza
kuwa kwa mapingamizi yaliyotolewa na kusababisha baraza lisiendee na
kazi yake kama ilivyopangwa inaonesha wazi ni jinsi gani vyombo vya
kusimamia maadili ya viongozi vinavyopuuzwa.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)