Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba
za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika hilo eneo la Napupa Mjini
Masasi.
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tunduru Bw. Paul Mkami(kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu
wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake ramani ya eneo la ardhi
lililopewa NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani
humo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC
Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakitembelea eneo la kujenga
nyumba za gharama nafuu Wilayani Namtumbo alipofanya ziara yake katika
Mkoa wa Ruvuma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua hatua zilizofikiwa
katika ujenzi wa Ofisi ya Shirika Mkoani Ruvuma ambapo ameagiza Ofisi
hiyo iwe imekamilika ndani ya mwezi mmoja ili kuwapa fursa wateja na
wananchi kupata huduma kwa urahisi. Kwa muda mrefu NHC haikuwa na Ofisi
ya kudumu katika Mkoa wa Ruvuma kutokana na sguli za Mkoa huo kusimamiwa
na Mkoa wa NHC wa Iringa.
Mradi wa nyumba za gharama
nafuu unaojengwa na NHC Wilayani Makete nao ulipata fursa ya kutembelewa
na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake.
Hapa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa Bw. Raymond Mndolwa
anaonyesha eneo ambalo litajengwa Kituo cha biashara ili kuhudumia
wakazi watakaoishi katika nyumba hizo za kisasa zinazouzwa kwa
wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Uendelezaji
Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio juu ya hatua za ukamilishaji wa mradi
wa nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo
alipotembelea mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2015.
Hali ya utekelezaji wa mradi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo inavyoonekana hivi sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakiukagua mradi wa nyumba za
gharama nafuu unaotekelezwa na NHC Wilayani Mbarali.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC
Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakiwa na Viongozi wa TRA Mkoa
wa Mbeya walipotembelea na kukagua maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa
majengo ya biashara katika Mpaka wa Tanzania na Zambia –Tunduma.
Taratibu zikikamilika NHC itajenga jingo la biashara katika mpaka huo
maarufu na muhimu kiuchumi. Picha zote na Muungano Saguya.