Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ambacho
kinapitia majina ya yaliopendekezwa kwenye nafasi za ubunge.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakipitia majina ya waliopendekezwa kwenye nafasi za Ubunge.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ,Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
mjini Dodoma kujadili majina ya waliopendekezwa kwa nafasi za Ubunge
kupitia CCM, kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na
Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula.
Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiwa kwenye mazungumza kabla ya
kuanza kwa kikao kutoka kushoto ni Dk. Salim Ahmed Salim, Mama Salma
Kikwete na Shamsi Vuai Nahodha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Dk.Salim Ahmed Salim kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
Mhe.Mwigulu
Lameck Nchemba akizungumza na Dk.Salim Ahmed Salim kabla ya kuanza kwa
kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC mjini
Dodoma.
Spika
la Bunge la Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Makinda akizungumza na Spika
wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho pamoja na
Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Khamis Juma kabla ya kuanza kwa kikao cha
Halmashauri Kuu mjini Dodoma.
Wajumbe wa NEC wakizungumza kabla ya kuanza kwa kikao, kutoka kushoto ni Ridhwan Kikwete, Mohamed Nyundo na Anthony Mavunde.
Katibu
wa NEC Uchumi na Fedha Mama Zakhia Meghji akizungumza na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kiakoa cha Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Katibu
wa NEC Uchumi na Fedha Mama Zakhia Meghji akizungumza na Katibu Mkuu wa
UWT Amina Mwakilagi kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza
kwa makini yanayoendelea kwenye kikao cha NEC, kulia ni Waziri Mkuu wa
Tanzania Ndugu Mizengo Pinda.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye.
Zaidi ya wajumbe 366 walihudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu wa
Tanzania Ndugu Mizengo Pinda wakati wa kikao cha NEC mjini Dodoma..