Mkuu
wa Shule ya Msingi Mkanyageni, Bwana Ramadhani Ngwali Makame, akitoa
neno la utangulizi wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni
10 baina ya shule hiyo na kampuni ya Zantel kanda ya Zanzibar.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo shuleni hapo.
Mkurugenzi
wa Biashara wa kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar, Bwana Mohamed Musa
akikabidhi hundi ya Shilingi millioni 10 kwa Mwenyekiti wa Shule ya
Msingi Mkanyageni, Bwana Ally Ngwali Vuai iliyoko visiwani Pemba kwa
ajili ya kukamiIsha ujenzi wa vyumba sita vya madarasa vitakavyotumiwa
na watoto zaidi ya 350. Anayeshuhudia ni Mkurugugenzi wa Mauzo Zantel,
Bwana Sukhwinder Bajwa pamoja na wanafunzi na wajumbe wa kamati ya shule
hiyo.
………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya
Zantel leo imetoa msaada wa shilingi milioni 10 kama mchango wa kujenga
madarasa sita katika shule ya msingi ya Mkanyageni iliyopo Pemba.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika
katika kumalizia ujenzi wa madarasa hayo sita kwa kuweka sakafu,
madirisha na milango, kupaka rangi pamoja na gharama za kazi kiujumla,
msaada ambao unatarajiwa kuboresha kiwango cha elimu katika shule hiyo.
Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi
wa Mauzo wa kampuni ya Zantel,Bw Sukhwinder Bajwa alisema msaada huo
umelenga kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wa shule hiyo.
‘Kampuni ya Zantel mara zote
imekuwa msitari wa mbele katika kuchangia kujenga nchi kwa kushiriki
katika kuwekeza katika shughuli za kijamii hasa katika sekta ya elimu
ambayo inaandaa mazingira na maisha bora ya viongozi wajao katika
upatikanaji wa elimu’ alisema Bwana Bajwa.
Akizungumza pia wakati wa
makabidhiano hayo, Mkurungezi wa Biashara wa Zantel upande wa Zanzibar,
Mohamed Mussa alisema Zantel imejikita zaidi katika kuhakikisha watoto
wanapata elimu bora visiwani hapa.
‘Kama kampuni inayoongoza kwa
idadi kubwa ya wateja visiwani hapa ni wajibu wetu kuhakikisha
tunajitolea kwa kuwekeza katika miradi inayogusa maisha ya wananchi kama
huu wa elimu ambao unaboresha miundombinu ili watoto wetu waweze kupata
elimu bora’ alisema Mussa.
Akitoa shukurani kwa kampuni ya
Zantel kwa msaada, Mwenyekiti wa kamati ya shule, Bwana Ali Ngwali Vuai,
alisema ni muhimu kuwekeza katika elimu kwani wanafunzi wakielimishwa
watakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa letu.
‘Tunawashukuru kampuni ya Zantel
kwa kutusaidia katika juhudi zetu kuhakikisha tunaboresha mazingira ya
elimu kwa watoto wetu’ alisema Bwana Vuai.