BFT yampongeza Rais wake Muta Rwakatale kwa kuchaguliwa kugombea udiwani kata ya CCM Kawe.

August 19, 2015
14. Baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM Kawe kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kamanda wa UVCCM Kawe,Aisha Voniatis na Mlezi wa Wazazi Muta Rwakatare
Baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM Kawe waliohudhuria kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kamanda wa UVCCM Kawe,Aisha Voniatis na Mlezi wa Wazazi Muta Rwakatare
……………………………………………………………..
Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) linatoa pongezi  za dhati kwa Rais  wa Shirikisho ndugu  ROBERT MUTA RWAKATALE  kuchaguliwa mgombea udiwani  kupitia CCM.
Katika  Kikao cha  kamati ya  utendaji  cha  (BFT)  kilichofanyika katika Ofisi  za  BFT kiliomba kumpongeza Rwakatale kwa nafasi hiyo aliyoipata kupitia chama cha CCM kwa kuchaguliwa kugombea Udiwani  KAWE.
BFT. Ina  Imani kubwa na uongozi wa MUTA  RWAKATALE kwa kuwa amekuwa  Imara kuhakikisha kuwa BFT inasonga mbele ingawa kuna changamoto mbalimbali za  kuongoza  vyama vya michezo.
 (BFT )  inaamini kuwa  endapo atachaguliwa kuwa Diwani KAWE  atashirikikana na Madiwa wa Kata nyingine pamoja na  Mbunge wa Kawe kuleta maendeleo ya haraka katika Jimbo la KAWE.
MUTA RWAKATALE amechaguliwa kwa kuwashinda vigogo waliogombea nafasi  hiyo  kama alivyokuwa MEYA wa  Manispaaa Kinondoni kwa miaka (10) na mjumbe wa NEC  SALUM  LONDA, OTHMAN  KIPETA- Diwani  ambaye amemaliza muda wake kwa sasa na Lokelo Willilo Makamu wa Rais (BFT).
MAKORE MASHAGA
KATIBU  MKUU ( BFT)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »