TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

August 19, 2015

download (8) 
KUZIONA AZAM Vs YANGA 7000 Mchezo wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba. Fuata link chini kwa taarifa kamili RATIBA VPL YATOKA, KUANZA KUTIMUA BUMBI SEPTEMBA 12 Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12 katika viwanja tofauti nchini na kumalizika Mei 7, 2016.
TFF inavisisitiza vilabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usjaili kesho alhamisi Agosti 20, 2015. Baada ya kufungwa kwa usajili huo hakutakua na muda tena wa nyongeza. Fuata link chini kwa taarifa kamili
TWIGA STARS KUWAAA HARAMBEE STARLETS JUMAPILI Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kushuka dimbani siku ya jumapili kucheza dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Starlets) katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar ukiwa ni mchezo wa kirafiki.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »