RADIO CALL ZA KISASA ZAINGIA NCHINI

August 19, 2015


Na Mwandishi Wetu,Globu ya Jamii
MAJANGA mbalilmbali nchini ambayo yamekuwa  yakitokea  na kushindwa kupata msaada ni kutokana na kuwa vifaa duni vya mawasiliano ya radio.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam wa Maonyesho na Mkutano wa Mawasiliano ya Radio za Kisasa ‘Radio Call’ 

Naibu Mkurugenzi wa Masafa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Libena Denis amesema kuwa kazi kubwa na kuona mawasiliano ya radio yanakua  na hivyo TCRA lazima isimamie.

Denis amesema kuwa kampuni ya Airsys  kuleta mawasiliano ya radio za kisasa na kuondokana na radio za kizamani ambazo kwa mabadiliko ya kitekonojia haziwezi kuhimili.
 
Aidha amesema  kuwa nchi za ulaya zimekuwa zikitumia mawasiliano hayo hivyo kuingia nchini itasaidia katika mawasiliano ya radio.

Amesema Meneja Mkuu wa  Airsys  Communication Technology Ltd,Sanctus Mtsimbe amesema mawasiliano ya matumizi ya radio yatakuwa nchini na kutoa urahisi wa upatikanaji wa huduma na mafunzo kwa wateja.

Amesema Tanzania imepewa kuwa kanda ya Afrika Mashariki  kwa kuwa na huduma ya Radio Call hivyo watumiaji watapata msaada na kuondokana na usumbufu wa kuagiza radio nje.
 Balozi wa marekani hapa nchini,Dianna Melrose akizungumza wakati wa kuzindua mkutano wa kampuni ya Airsy katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
 Afisa mtendaji mkuu,Hans Beckers akionyesha redio call ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Airsy ambazo zitakuwa zikisaidia katika ulinzi katika nchi mbalimbali ambazo zitakuwa zikisambazwa hapa nchini alionyesha redio hizo katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam leo.
 Naibu Mkurugenzi wa Masafa wa Mamlaka ya mawasiliano (TCRA), Libena Denis akizungumza katika mkutano wa kuwaonyesha watanzania jinsi redio hizo zinavyo fanya kazi katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
 Baadhi ya waliohudhulia katika mkutano.
 Meneja wa mauzo wa kampuni ya Airsys,Raurent Tribout akitoa maelezo kuhusiana na mauzo ya redio kalu hizo.
Msemaji wa kampuni ya Airsys, Sanctus Mtsimbe akizungumza na waandishi wa habari leo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa mtendaji mkuu,Hans Beckers wa kampuni ya Airsy.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »