KESSY HASSANI MWENYEKITI MPYA AFRICAN SPORTS”

August 18, 2015
ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa timu ya African Sports
“Wanakimanumanu”katika uongozi uliomaliza muda wake, Hassani Kessy amechaguliwa kushika wadhifa wa Mwenyekiti wa Klabu hiyo baada ya kupata kura 52 ambao ni sawa na asilimia mia moja kwenye uchaguzi mkuu.

Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Spended na kusimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Wakili Aloyce Komba ambaye aliwataka viongozi ambao wamechaguliwa kuchangia kasi ya maendeleo kwenye timu hiyo ili iweze kurudisha makali yake ya miaka ya nyuma.

Kessy ambaye aliwania nafasi hiyo akiwa hana mpinzani alifanikiwa kupata kura kwa njia ya ndio na hapana ambapo kati ya wajumbe 53 kuwa moja iliharibika kwenye mchakato huo wa uchaguzi.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichaguliwa aliyekuwa Meneja wa timu hiyo,Abdul Ahmed ambapo alipata kura za ndio zote ambapo alikuwa hana mpinzani kwenye mchakato huo wa uchaguzi.

Aidha kwa upande wa wajumbe wa kamati ya utendaji walifanikiwa
kuchaguliwa Godias Kimath aliyepata kura (51), Mwinshame Mbwana aliyepata kura (52) na Abdallah Babala aliyepata kura (51)waliopata kuwa za ndio kwenye mchakato huo ambao Kamati hiyo iliiagiza klabu hiyo kuhakikisha inajaza nafasi mbili za wajumbe waliosalia ili iweze kutimia idadi ya watano ambao wataunda kamati ya utendaji.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa,Kessy alisema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarudisha makali yake ya miaka ya nyuma wakati walipopanda daraja na kufanikiwa kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »