Katibu Tawala Mkoa Mkoa wa
Lindi,Abdallah Dadi Chikota ambae hivi Karibuni Alichaguliwa na Wana CCM
kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Nanyamba Mtwara na Kupitishwa na
Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM Kuwania Jimbo Hilo akiwaaga wakuu
wa Idara na Vitengo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Wakuu wa Idara na Vitego Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika Kikao kazi Ambapo Katibu Tawala wa
Mkoa wa Lindi alitumia Fursa kuagana na wasaidizi wake.
…………………………………………………
Na ABDULAZIZ ,Lindi
Wafanyakazi wa Sekriterieti ya
Mkoa wa Lindi wametakiwa Kudumisha mshikamano na Ushirikiano katika
Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo Inayotekelezwa na ikiwemo
mchakato wa Ujenzi wa Wodi ya Kisasa na Nyumba ya Ghorofa kwa Madaktari
wa Hospital ya Mkoa wa Lindi Ujenzi unaotarajiwa Kuanza
Wito huo Umetolewa Jana na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Lindi,Abdallah Dadi Chikota alipokuwa akiwaaga Wakuu
wa Idara Na Vitengo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kufuatia Kushinda
Katika Kura za Maoni na Kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kuwania Ubunge
katika Jimbo la Nanyamba Mkoani Mtwara
Uteuzi wa CCM NA Baadae kuteuliwa
na Tume ya Uchaguzi itamfanya Katibu Tawala huyo Kukoma Rasmi Ajira ya
Utumishi wa Umma Serikalini kwa Mujibu wa Taratibu za Kiutumishi
Akiongea na Wakuu hao,Chikota
ambae katika Uongozi wake Alifanikiwa Kuunganisha Watumishi wake
kufuatia Uwepo wa Makundi aliyoyakuta kutokana Na Mgogoro Uliokuwepo
kutokana Migongano ya Kiutendaji iliyokuwepo katika Sekriterieti Hiyo
Aidha Chikota aliwataka Watumishi
wa Serikali Kumpa Ushirikiano Mkubwa Bw Grayson Mwaigombe ambae
atakakuwa Akikaimu Nafasi Hiyo anayoicha ambapo alisisitiza Kufanya kazi
kwa kufuata Mifumo ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradi na Fedha
Miradi kutumika kama ilivyooanishwa katika Bajeti ya Serikali
‘Watumishi wenzangu Nawashukuru
sana kwa Ushirikiano Mlionipa kwa kipindi chote nilichokuwa nanyi Naomba
Kuwasisitiza ni lazima ili kufikia mafanikio lazima Muwe na Vikao vya
Mara kwa Mara kupeana Mrejesho na Muhimu kuzingatia Fedha za Miradi
zitumike kwa kufuata Utaratibu na Miongozo Iliopo kwa Manufaa ya UMMA na
isiwe kwa Ajili Binafsi ‘Aliwasihi Chikota
Katika Uongozi wake miradi
aliyoicha katika Utekelezaji ni Pamoja na Nyumba ya Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Kilwa,Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Nyumba za
maofisa Tarafa pamoja na Ujenzi wa Wodi ya Kisasa na Nyumba ya Ghorofa
kwa ajili Ya Madaktari wa Hospital ya Mkoa wa Lindi na Ukarabati wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Nae Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Lindi,Grayson Mwaigombe kwa Upande wake alieleza kuwa ataendeleza
Mipango Yote Iliyoachwa na Chikota kwa kukamilisha Miradi ambayo Imeanza
na Ile ambayo Imepangwa Inasubiri Pesa Toka Hazina Huku akizitaka
Halmashauri zote Kutekeleza agizo la Serikali la Kutumia Asilimia 60 YA
Mapato ya Ndani kwa Miradi ya Maendeleo kusaidia utoaji wa Huduma za
Jamii Ikiwemo Ujenzi wa Maabara,Vyumba Vyumba vya Madarasa,Numba za
Waganga na Zahanati na Vituo Vya Afya Katika Mkoa huo
Chikota kabla ya Kuteuliwa kuwa
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi alipitia Nyadhifa Mbalimbali Ikiwemo Afisa
Elimu wilaya,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Newala Hivi
karibuni katika Mchakato wa Kutafuta Mgombea Ubunge Aliomba Ridhaa
hiyo ambayo alishinda kwa Kishindo katika Uchaguzi wa CCM Jimbo la
Nanyamba na Kupitishwa na Kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM kuwania
Nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu Ujao