BIMA YA AFYA (NHIF) YAWANOA WANACHAMA WAANDISHI WANAWAKE MKOA WA TANGA (TWMO)

August 15, 2015





Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi  Wanawake Mkoa wa Tanga (TWMO) Betha Mwambelwa, akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa kongamano la siku moja la Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya  (NHIF) kuwajengea uwezo namna ya kujiunga na mfuko huo wa matibabu bure kwa malipo kdogo kongamano lililofanyika leo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.



 Mkurugenzi wa Mifuko ya Afya ya Jamii kutoka Makao Makuu,(NHIF) Eugen Mikongoti, akitoa maelezo kwa Wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Tanga (TWMO)  wakati wa kongamano la siku moja la kuwajengea uwezo wa kujiunga na mfuko huo wa matibabu bure mwaka mzima kwa malipo kidogo kongamano lililofanyika leo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.





 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Hafsa Mtassiwa (kulia) , akipokea mashuka 100  kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa Mifuko ya Afya ya Jamii Makao makuu, Eugen Mikongoti, kwa ajili ya wodi ya wanawake na watoto kujikinga na malaria wakati wa kongamano la siku moja la Wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Tanga lililofanyika leo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga , kushoto ni Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga, Ali Makababu.


 Wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Tanga (TWMO), wakifuatilia kwa makini elimu ya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kongamano lililofanyika leo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga
 Wanachama wa Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Mkoa wa Tanga, (TWMO) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtassiwa na viongozi wengine wa Biama ya Afya kutoka Mkoani na Makao makuu


 Bosi wa Mwananchi Communication Ltd (MCL) Mkoa wa Tanga, Salma Miraji (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtassiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mifuko ya Jamii Makao Makuu Dar es Salaam, Eugen Mikongoti (katikati) mara baada ya kumalizika kongamano la siku moja la Chama Cha Waandishi Wanawake Mkoa wa Tanga (TWMO) lililofanyika leo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga
MENEJA MASOKO wa Mwananchi Communicatio Ltd (MCL)Mkoa wa Tanga, Salma Miraji (kushoto) akiwa na msaidi wake, Cecylia wakifuatilia kwa makini kongamano la siku moja la Chama Cha Waandishi wa Hbari Wanawake juu ya kujengewa uwezo wa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) lililofanyika leo, Wilayani Korogwe Mkoani Tanga


 Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi  Wanawake Mkoa wa Tanga (TWMO) Betha Mwambela kulia akiwa picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa mara baada ya kumalizika semina ya mfuko wa Bima ya Afya leo wilayani humo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »