Kikosi cha Taifa Stars Maboresho
kimeingia kambini leo (Desemba 1 mwaka huu) Bulyanhulu mkoani Shinyanga
kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9
mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij,
Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo hadi Desemba 6 mwaka huu
ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo
itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioingia kambini ni
Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally Mohamed (White Bird), Aishi
Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Atupele Green (Kagera
Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda (African Lyon).
Gadiel Michael (Azam), Hashim
Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba), Hassan Mwasapili (Mbeya
City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed Simbaulanga (African Lyon),
Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally (Mtibwa Sugar).
Miraji Adam (Simba), Mohamed
Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda),
Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Said Hamisi
(Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza Ramadhan (Mtibwa
Sugar).
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba madini ya Acacia Mining
PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa kufadhili kambi ya Stars
kupitia mgodi wa Bulyanhulu.
EmoticonEmoticon