Kiungo Emerson De Oliveira Neves Roque leo
amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Young Africans baada
ya benchi la ufundi kuridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe
kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.
Baada ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha
Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward,
Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe
kandarasi la kuitumikia klabu ya Young Africans.
Emerson aliyekua
akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo
la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja"
ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na
kuomba klabu ya Young Africans imuache.
Kocha wa Young Africans
Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na
kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na
Kimataifa.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans
kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni
Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.
EmoticonEmoticon