AJALI ZA BARABARANI ZAONGEZEKA TABORA ZAUWA IDADI KUBWA YA WATU!

December 01, 2014

Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akipata maelezo kutoka kwa Dr.Anna Kichambati wa Redcross Tabora wakati wa sherehe za wiki ya usalama barabarani mkoani Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akisalimiana na Afisa mfawidhi wa Sumatra mkoa wa Tabora Bw.Joseph Michael wakati wa wiki ya usalama barabarani mkoa wa Tabora
Mmoja kati ya maafisa wa polisi kikosi cha usalama barabarani Tabora mjini akimuonesha mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila kifaa maalumu kinachotumika kupima kiwango cha ulevi kwa madereva wazembe.(P.T)
Kikosi cha zimamoto mkoa wa Tabora kikionesha vifaa vinavyotumika wakati wa uokoaji ajali zinapojitokeza.
Sherehe za wiki ya usalama barabarani mkoa wa Tabora zilianza kwa maandamano yaliyopita mitaa mbalimbali hadi viwanja vya mazoezi ya Jeshi la Polisi Tabora ambapo wananchi walishiriki maandamano hayo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kikosi cha usalama barabarani SSP Peter Mnyandwa akitoa taarifa ya ongezeko la  ajali za barabarani mkoani Tabora ambapo zaidi ya watu 150 wamefariki dunia katika ajali 399 huku watu 520 wamejeruhiwa katika ajali 185.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akihutubia katika sherehe hizo za wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambapo mbali ya kusikitishwa na taarifa ya ajali hizo lakini alisema kuwa asilimia 75 ya ajali hizo zinatokana na makosa ya kibinadamu na hivyo kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua ya kudhibiti kupunguza ajali hizo ikiwa ni pamoja na kutotoa leseni kwa madereva ambao hawajapata mafunzo ya udereva darasani.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti mstaafu wa Kamati ya Usalama barabarani mkoa wa Tabora Bw.Moshi Abrahamu maarufu Nkonkota.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akikabidhi cheti cha pongezi kwa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya NBS kwa usafirishaji salama bila kusababisha ajali kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »