Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji yafanya Mahafali ya Sita

December 01, 2014

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye miwani) akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa wahusika alipotembelea labaratori ya mitambo ya maji katika Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) kabla ya kuudhuria maafali ya sita ya Taasisi hiyo hivi karibuni. unnamed1 
Baadhi ya wahitimu kutoka Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) wakiwa katika maandamano ya kitaaluma wakati wa Maafali ya sita cha Taasisi hiyo hivi karibuni.
unnamed3 
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Dkt. Shija Kazumba (kushoto) akimkaribisha Mgeni rasmi katika maafali ya sita ya Taasisi hiyo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mgeni rasmi wa mahafali hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwahutubia wahitimu (hawapo pichani) wakati wa mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI). Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Dkt. Shija Kazumba na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Prof. Gabriel Roderick Kassenga. unnamed5 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea risala ya wahitimu iliyosomwa na kuwasilishwa kwa mgeni rasmi na Bw. Magembe Maduhu.
unnamed6 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimpa tuzo mhitimu aliyeongoza katika kundi la wanawake na aliyekua na ufaulu mkukwa kuliko wahitimu wote Bi. Fatma Ngano, kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Dkt. Shija na ushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Prof. Gabriel Roderick Kassenga.
unnamed7 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ambaye pia ni mgeni rasmi katika mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye miwani) katika picha ya pamoja na wakufunzi na wahitimu wa Taasisi hiyo.
unnamed8 
Kikundi cha ngoma kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania Mwenge wakitumbuiza wakati wa mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WDMI) yaliyofanyika hivi karibuni.
 Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »