NAIBU Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga,Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi mabati 50 Mkuu wa wilaya ya Pangani,Hafsa Mtasiwa ikiwa ni jitihada za kuunga mkono ujenzi wa maabara unaondelea maeneo mbalimbali hapa nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalumu(CCM)mkoa wa Tanga,Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi kadi Bi Halima Kassim mmoja wa wanachama wapya kwenye kata ya Maramba wilayani Mkinga. |
Na Amina Omari,Mkinga
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummi Mwalimu ametoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh Milioni moja na nusu kwa wilaya mbili za Mkinga na Pangani kusaidia ujenzi wa maabara.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummi Mwalimu ametoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh Milioni moja na nusu kwa wilaya mbili za Mkinga na Pangani kusaidia ujenzi wa maabara.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mifuko 70 ya saruji kwa wilaya ya Mkinga na mabati 50 kwa wilaya ya Pangani.
Akikabidhi vifaa hivyo Naibu waziri alisema kuwa lengo
kubwa ni kuunga mkono agizo la Rais la ujenzi wa maabara kwa shule zote
za sekondari nchini.
"Nimeona na mimi kama waziri mwenye thamana na mwananchi
wa Mkoa wa huu kusaidia kuharakisha ujenzi wa maabara katika wilaya hizi
mbili"alisema Naibu waziri Mwalimu.
Pia aliongeza kuwa nia ya serikali kuagiza ujenzi wa
maabara ni kutaka wanafunzi wanaochukuwa masomo ya sayansi kupata fursa
ya kufanya mazoezi kwa vitendo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mkinga Mboni Mgaza
alishukuru kwa msaada wa mifuko ya saruji na kusema utasaidi kuharakisha
ujenzi huo.
Pia aliongeza kuwa tayari ujenzi wa vyumba vya maabara
katika wilaya hiyo umefikia katika hatua nzuri kwani ziadi ya asilimia
70 ya ujenzi imekamilika.
Vile vile mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa alimpongeza Naibu waziri kwa juhudi zake za kuwaunga mkono kwenye ujenzi huo.
"Kwa msaada huu kwa wilaya ya Pangani tutakuwa
tumekamilisha kuezeka vyumba vilivyokuwa havijaezekwa na tunaimani
tutakamilisha kwa wakati ujenzi wa maabara"alisema Dc Mtasiwa.
Picha kwa Hisani ya Katibu wa Naibu Waziri,Lulu Mussa
Picha kwa Hisani ya Katibu wa Naibu Waziri,Lulu Mussa
EmoticonEmoticon