WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WADAU WA MADINI YA SHABA

November 25, 2014

unnamedKamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Wengine kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uongezaji Thamani Madini, Latifa Mtoro na Mwakilishi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Mvumula.
unnamed2Mfanyabiashara wa madini ya Shaba kutoka Kanda ya Kati Doreen Kisia, akisistiza jambo wakati akichangia hoja katika mkutano huo.
unnamed3Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, akiongea jambo wakati akichangia mada kuhusu madini ya Shaba.
unnamed4Kamishna Msaidizi  Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, akisalimiana na baadhi ya wadau wa madini ya Shaba waliohudhuria mkutano huo.
unnamed5Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, (kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano huo

………………………………………………………………………….
Na Asteria Muhozya, Dare s Salaam
Wizara ya Nishati na Madini imekutana na wadau wa madini ya Shaba katika mkutano wa siku mbili ulioanza tarehe 24- 25 Novemba, 2014 na kuwashirikisha wafanyabiashara wa madini hayo, wachimbaji wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishana Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.
Akifungua mkutano huo, unaolenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ndogo ya madini ya Shaba na namna ya kuyaongezea thamani madini hayo, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja amewataka wachimbaji wadogo nchini kutumia fursa zinazotolewa na Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo kupata ruzuku ili waweze kuendeleza shughuli za uchimbaji wa madini jambo ambalo litasaidia kuyaongezea thamani madini hayo.
Aidha, Kamishna Masanja ametumia fursa hiyo, kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kinyume na sheria na taratibu kwa kuwa jambo hilo linaikosesha Serikali mapato ikiwemo kuchangia madini hayo kutokupata thamani halisi.
Vilevile Kamishna Masanja ameeleza kuwa, Serikali itaendelea kuzuia usafirishaji madini ghafi ya Shaba na kueleza kuwa, “Haturuhusu madini ghafi ya shaba kutoka nje, tunataka yatoke yakiwa tayari ni madini, kwasababu kuna zaidi ya shaba hivyo tunapoteza, tunataka kuyaongeza thamani madini yetu hapa hapa nchini”, alisisitiza Masanja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »