WIZARA ya Mifugo na Uvuvi Tanga
imetakiwa kuongeza doria katika pwani ya bahari ya Hindi kuzuia vitendo vya uvuvi haramu wa mabomu na
utupa lengo likiwa ni kulinda rasilimali
za viumbe hai baharini.
Rai hiyo imetolewa na washiriki wa mashindano ya wavuvi
wa samaki yaliyodhaminiwa na kiwanda cha Saruji cha Simba Cement (TCCL) na kusema kuwa samaki wengi wametoweka kufuatia kushamiri kwa uvuvi haramu.
Alisema samaki wengi
wamepotea na viumbe hai vya baharini kufa kufuatia uvuvi huo ambao umekuwa
ukifanyika nyakati za usiku na hivyo kuitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kulikomesha
“‘Boti yetu imeweza kutembea hadi karibu na pwani ya wavuvi
kisiwani Pemba na tumerejea na samaki
mmoja tu kwa kweli ni aibu---tulikuwa na vifaa vya kisasa vya kuvulia”
alisema na kuongeza
“Sababu ni kuwa bado vitendo vya uvuvi haramu vipo jambo
linaloashiria miaka mitano Tanga haitakuwa na samaki na hivyo ni wajibu ya mamkala
kulikomesha” alisema Asif Ganighee
Alisema kipindi cha nyuma Tanga ilikuwa kituo kikuu cha
uvuaji wa samaki na kuwavitia wachuuzi wa ndani na nje ya nchi na hivyo kuitaka
kurejeshwa kwa hali hiyo na kuwezesha uchumi wa Mkoa na wananchi kupanda.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa kiwanda cha Saruji cha Simba
Cement, Mtanga Noour, aliwataka washiriki hao kuwa mabalozi wazuri kwa wavuvi
wengine ili kuwaweka pamoja na kuzungumza changamoto zinazowakabili.
Alisema wavuvi wengi wamekuwa wakikumbana na changamoto
nyingi za baharini na nje ya bahari na
hivyo kuyataka mashindano hayo kuwa chachu ya kuwashirikisha wengine mwakani.
“Sekta ya uvuvi iko na changamoto nyingi na nadhani hakuna
kiwakutanishacho kama hiki cha leo----kwa kweli kama tutakuwa na utaratibu kama
huu sekta hii itakuwa ni yenye maendeleo” alisema Mtanga
Alisema kiwanda cha Saruji kimekuwa kikisaidia makundi mbalimbali
ya kijamii pamoja na sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha kufanya kazi zao kwa
ufanisi na kuwa wavuvi bora na wa kisasa.
Aliwashauri kila mmoja kuwa askari wa mwenzake katika
kukabiliana na uvuvi haramu wa upigaji wa mabomu na utumiaji wa nyavu aina ya
kokoro pamoja na utupa ili kuurejesha Mkoa huo katika uvuvi wake wa asili.
EmoticonEmoticon