TANGA.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Subira Mgalu
amezionya timu ambazo zinashiriki kwenye michuano ya Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi Nchini (SHIMUTA) kuacha kuchukua wachezaji
ambao sio wafanyakazi kwani kufanya
hivyo wanapunguza ladha ya mashindano hayo.
Mgalu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati
akizundua mashindano ya Shimuta yanayofanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani
mkoani hapa na kushirikisha wanamichezo wapatao 500 kutoka mashirika na
makampuni mbalimbali hapa nchini.
Alisema kuwa michezo hujenga undugu na furaha baina
ya wanamichezo hivyo kuwaingia wachezaji ambao sio wafanyakazi kwenye
mashindano hayo wataondoa maana halisi ya mashindano hayo jambo ambalo linaweza
kuwafanya kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea
“Mashindano
haya ni ya wanamichezo wafanyakazi…kuna wale wanamichezo ambao sio wafanyakazi
ambao wanajulikana kama mamluki au wavamizi kwamba hapa sio mahala pao nawasihi
tuchezeshe wafanyakazi halisi ili mshindi apatikane kihalali na sio vyenginevyo…..
kwa sababu ni hatari sana kumleta mwanamichezo ambaye sio mfanyakazi kwenye
michezo hii anaweza kuvunjika mguu au akifa kwa mfano hatuombei itokee hiyo
itakuwaje “Alisema DC Mgalu.
Aidha alizitaka timu hizo kuacha kuwatumia wachezaji
wa aina hiyo kwani wana madhara makubwa hasa pale yanapokuwa yakijitokeza kwa
kuzitaka timu zenye utamaduni huo kuhakikisha wanaondokana nao.
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya alionekana kukerekwa
na baadhi ya menejimenti za Taasisi,Mashirika na makampuni mbalimbali kuwa na
utashi wa kutokupenda michezo na wengine kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha
kuacha kufanya hivyo badala yake wamuunge mkono Rais Jakaya Kikwete katika
jitihada zake za kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini.
Akizungumzia waamuzi wanaochezesha mashindano
hayo,DC Mgalu aliwataka kuchezesha kwa haki bila upendeleo kwa kufuata sheria
za mchezo husika ili mshindi aweze kupatikana kihalali kwa sababu wakienda
kunyume chake wanaweza kusababisha tafrani na manung’uniko kwa baadhi ya timu
shiriki.
Hali kadhalika aliwataka kuhakikisha wanakuwa na
nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano ikiwemo kukubaliana na matokeo
pindi watakapojikuta wamefungwa wakati wa mashindano hayo.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu huyo wa
wilaya, Mwenyekiti wa Shimuta, Khamis Mkanachi alisema kuwa mashindano hayo
msimu huu yanashirikisha timu 20 pungufu ya 22 zilizoshiriki mwaka jana mkoani
Dodoma ingawa walijiwekea lengo la kuwa na timu 25 hadi 30 mwaka huu .
Alisema kuwa kupungua kwa idadi ya timu shiriki
kunatokana na baadhi ya mashirika kubinafsishwa hali ambayo imepelekea timu
nyingi kushindwa kupata nafasi ya kupeleka washiriki wake lakini pamoja na
kuwepo hali hiyo shirikisho hilo limendelea na jitihada za ziada kuhakikisha
idadi ya timu hizo haipungui bali kuongezeka.
Aidha alizitaja timu hizo kuwa ni Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC),Chuo Kikuu Huria(OUT),Chuo cha Elimu ya
Biashara(CBE),Kampasi za Mbeya na Dar es Salaam na Mwanza,Shirika la Umeme
Tanzania(TANESCO),Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Chuo Kikuu cha Ardhi.
Timu nyengine ambazo zinashiriki mashindano hayo ni Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA), Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini(IRDP),Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA),Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MOCU),Chuo kkikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS),Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Wengine ambao watashiriki kwenye mashindano hayo ni Baraza la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira (NEMC),Shirika la Mzinga,Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC), Wenyeji wa Mashindano hayo,TANGA CEMENT na Timu mpya kwenye shirikisho hilo ya Bohari ya Madawa(Medical Stores Department(MSD).
Timu nyengine ambazo zinashiriki mashindano hayo ni Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA), Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini(IRDP),Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA),Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MOCU),Chuo kkikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS),Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Wengine ambao watashiriki kwenye mashindano hayo ni Baraza la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira (NEMC),Shirika la Mzinga,Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC), Wenyeji wa Mashindano hayo,TANGA CEMENT na Timu mpya kwenye shirikisho hilo ya Bohari ya Madawa(Medical Stores Department(MSD).
EmoticonEmoticon