Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika
mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete
anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa
maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais
Profesa .Mohamed Janabi
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika
mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete
anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa
maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais
Profesa .Mohamed Janabi
………………………………………………………………….
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI LEO
Taratibu za matibabu ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.
Taratibu hizo za matibabu za
Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo
wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini
Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya
tiba.
Hata hivyo, Rais Kikwete
ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na
Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza
safari ya kurejea nyumbani.
Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.
Rais Kikwete aliondoka nchini
Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake
lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia
upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete anaendelea
kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona
haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Novemba,2014
EmoticonEmoticon