Katibu
mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa
Ndugu Sixtus Mapunda amepata makubwa wilayani Mbinga yaliyoacha gumzo
kubwa wilayani hapo. Mapunda ambaye alitoke wilaya ya Nyasa amepokelewa
kwa kishindo kikubwa na viongozi wa CCM pamoja na mamia ya wananchi wa
wilaya ya Mbinga ambako ndipo alikozaliwa.
Mapunda
ameingia Mbinga jana akitokea wilaya ya Nyasa ambapo ni muendelezo wa
ziara yake ya siku tano (5) Mkoani Ruvuma. Ziara ambayo inalenga kukagua
na kuhamasisha ujenzi na uimara wa jumuiya mkoani humo pamoja na
kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi ya mwaka
2010-2015.
Katika
hotuba yake Katibu Mkuu amewataka wananchi wa Mbinga kujitokeza kwa
wingi na kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi katika
uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotegemewa kufanyika mapema mwezi ujao
pamoja na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.
Pia
Katibu Mkuu, Mapunda amemtembelea Mzee Constantine O. Millinga mmoja wa
waasisi kumi na watano (15) walioanzisha Chama Cha Ukombozi cha TANU
wakiongozwa na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
mnamo tarehe 7.7 1954. Mzee Millinga ni miongoni mwa wawili kati ya
waasisi hao ambao wako hai mpaka hivi sasa.
Mapunda
ametoa wito kwaWatanzania, wananchama wa Chama Cha Mapinduzi na hasa
Vijana wa Taifa hili, kuwaenzi na kuwatembelea wazee ambao ni waasisi,
wazalendo wa kweli na wapigania uhuru wa nchi hii, ambao wametuwekea
misingi ya Umoja na Utaifa ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya amani
na utulivu.
Katibu
Mkuu huyo wa UVCCM anaendelea na ziara yake Mkoani Ruvuma ambapo
atatembelea wilaya ya Namtumbo na baadae Songea Mjini ambako atahutubia
mkutano mkubwa wa hadhara katika wilaya hiyo ambayo ni makao makuu ya
Mkoa wa Ruvuma.
EmoticonEmoticon