Ni
habari ya kusikitisha sana kupata taarifa hizi kwa kila mwenye moyo wa
binadamu. Mtoto huyu ambaye alioneshwa akiteswa na house girl katika
video iliyorekodiwa kwa siri na camera iliyotegeshwa sebuleni bado yupo
katika hali mbaya.
Mtoto
alivunjika mbavu kutokana na kukanyagwa sehemu ya mbavu zake. Hivi leo
tu tulipost video inaonesha jinsi ambayo mtoto huyu alikuwa
akilazimishwa kula wakati akilishwa chakula kwa namna ya kikatili, na
kishwa kupigwa na kukanyagwa mara tu alipotapika kutokana na kulishwa
chakula kingi na kwa haraka.
Hizi ni habari za kusikitisha sana mtoto mzuri kama huyu malaika
asiye na makosa kunusurika kukatizwa maisha yake kwenye mazingira kama
haya. Mwandishi wetu anazidi kusisitiza juu ya umakini kwa wazazi na
walezi wote kuwa makini katika kuwafahamu vizuri watu wanaowaachia watu
wanaowaachia majukumu ya kuwalea watoto wao.
Ni vyema kujipatia uhakika juu ya tabia za wasaidizi hawa wanaofanya
kazi ya kushinda na kulea watoto wetu wakati wote ambao tunakuwa katika
majukumu mengine ya kila ili kuweza kuendesha maisha yetu.
Ni kweli kwamba hatuwezi kufanya haya majukumu wenyewe bila usaidizi
wa mabinti wa kazi. Wao ni muhimu na msaada mkubwa katika kuhakikisha
kwamba watoto wanabaki salama na shughuli nyinginezo zinaendelea kama
kawaida katika kuendesha maisha ya yetu na familia kwa ujumla. Lakini
imetupasa kuwa makini kutokana na matukio kadhaa ya ukatili wa jinsi hii
kwa watoto. Ni vyema kujua kwa undani tabia na mazingia ambayo msaidizi
huyu amelelewa na kukua, na kupafahamu mahali anapotokea na ndugu zake.
EmoticonEmoticon