KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS WAKIPEWA NASAHA BAADA YA KUMALIZIKA MECHI HIYO LEO |
KATIKATI NI THE BIG BOSI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,HEMED AURORA NA KULIA NI KOCHA WA VILLA SQUAD HABIBU KONDO NA KUSHOTO NI MTANGAZAJI WA TK FM SAAMAMY MOHAMED |
KATIKATI NI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,HEMED AURORA NA KUSHOTO NI KOCHA WA TIMU YA MGAMBO SHOOTING,BAKARI SHIME NA KULIA NI KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI LEO |
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
MABAO Mawili yaliyofungwa na Hassani Materema kunako dakika za 18 na 79 yalitosha kuweza kuwapa ushindi timu ya African Sports wa Mabao 2-1 dhidi ya Villa Squad katika mchezo wa Ligi daraja la kwanza uliochezwa leo uwanja wa CCM Mkwakwani.
African Sports ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lake katika dakika ya 18 ambalo lilifungwa na Hassani Materema baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Villa Squad kabla ya Villa Squad kusawadisha dakika ya 36 kupitia Omary Masha.
TImu zote zilikwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote ziliingia uwanjani hapo zikiwa na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi wa wachezaji wake.
Wakionekana kujipanga vilivyo,African Sports waliweza kuongeza wimbi la mashambulizi langoni mwa Villa Squad na kufanikiwa kuandika bao la pili dakika ya 79 ambalo likifungwa na Hassani Materema.
EmoticonEmoticon