Na Salum Mohamed,Pangani,
WAKAZI wa kijiji cha Mkalamo Wilayani
Pangani Mkoani Tanga, wamesema wamechoshwa na ahadi ya Serikali kuwachimbia
kisima cha maji safi kijijini hapo na hivyo kuadhimia kuchangishana na kuchimba
kwa gharama zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa blog hii,
wakazi hao walisema kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikitoa ahadi hewa za kuchimba kisima lakini hadi muda huo
hakuna dalili zozote za utekelezaji.
Walisema kufuatia kusuasua huko na wakazi wengi eneo hilo kuteseka kwa kuyafuata maji umbali
mrefu na kuamua kuchangishana kwa kila nyumba kuchangia elfu 20 na kufikisha
lengo ambalo wamejiwekea.
“Kipindi kirefu tumekuwa tukiahidiwa kuchimbiwa kisima na
hata viongozi wa ngazi za juu nao ni wamoja wapo----hadi sasa hakuna dalili ya
ahadi hiyo na kuamua ni vyema tukachangishana wenyewe kwa wenyewe” alisema
Rashid Sinani
“Kero tunaijua sisi wenyewe na sio wakuja na ndio maana
tunataka kuchangishana wenyewe kwa wenyewe---tuko na imani kuwa tutachimba
kisima kwa nguvu zetu” alisema Sinani
Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Perani, Juma Kolombo amewashauri
viongozi wa Serikali za vijiji na vitongoji kuzifikisha kero za wananchi katika
ngazi husika na kuacha kuzikalia katika makabati.
Alisema kuna baadhi ya viongozi wengi wanashindwa kuwajibika
na badala yake wamekuwa mzigo kwa wananchi na hivyo kuwataka kubadilika
vyengine mkakati wa kuwondosha kwa vikao vya vijiji utafuatwa.
“Kuna viongozi wamekuwa mzoigo wanashindwa hata kupeleka
barua za wananchi ngazi za juu---hiyo nadhani ni woga wa kupoteza kibarua chake
lakini hatambui kuwa ndio kuwajibika” alisema Kolombo
Aliwataja viongozi hao kuwa ni mzigo kutokana na kutofikisha
kero zao hata ngazi za kijiji na hivyo kuona kuwa kibarua ambacho wamepewa na
wananchi kupitia masanduku ya kura kimewashinda.
Alisema kipindi cha kufanya hivyo ni chaguzi za Serikali za
mitaa ambazo ziko karibu na hivyo kuwataka kuwajibika na kuonyesha moyo kabla ya
kipindi hicho kufika vyengine wananchi wanaweza kufanya maamuzi tofauti na
wanavyofikiria.
chanzo:kumekuchablog
chanzo:kumekuchablog
EmoticonEmoticon