NA MWANDISHI WETU,KILINDI.
IMEELEZWA
kuwa chanzo cha tukio la kuungua moto nyumba mmoja yenye fremu nne za maduka
wilayani Kilindi mkoani Tanga ilisababishwa na moto ulikuwa ukitumiwa na mama
lishe jirani eneo hilo kusambaa kwenye maeneo yaliyopo sheli hiyo na kuunguza
eneo hilo.
Moto
huo uliachwa bila kuzimwa baada ya mamalishe hao kumaliza biashara zao za kuuza
chakula jambo ambalo lilipelekea kuleta hasara kubwa kwenye maduka hayo ambapo
thamani yake bado haijajulikana mpaka sasa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai alithibitisha kutokea tukio hilo ambapo
alisema lilitokea Octoba 7 mwaka huu katika kijiji na kata ya Negero Tarafa ya
Kimbe wilayani humo .
Akielezea
jinsi tukio hilo lilivyotokea Kamanda Kashai alisema kuwa gari lenye namba za
usajili T.219 AUC Center yenye tanki la mafuta linalomilikiwa na Adolf Lykundi
mkazi wa Handeni lilishika moto na kulipuka wakati likimimina mafuta ya petrol
kwenye mapipa dukani kwa Majaaliwa Songomelo.
Hata hivyo,Kamanda Kashai alisema kuwa katika
tukio hilo hakuna madhara yaliyotokea kwa binadam.
Wakati
huo huo,mkazi mmoja wa Kijiji cha Mafisa Kata ya Mvungwe Tarafa ya Mgera
wilayani Kilindi ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya
Tumboni, Shingano na Kichwani hali iliyopelekea kufariki dunia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai alithibitisha kutokea tukio hilo ambalo
lilitokea Octoba 7 mwaka huu saa 11:30 Marehemu akiwa shambani kwenye kitongoji
baina ya Kijiji cha Mafisa wilayani humo.
Kamanda
Kashai alimtaja alifariki dunia kwenye tukio hilo kuwa ni Lokoye Machaku (29)
kabila Mnguu mkazi wa Maafisa wilayani humo ambayo alichomwa kitu chenye ncha
kali sehemu mbalimbali kwenye mwili wake.
Aidha
alisema kuwa wakati huo mtu mwengine aliyekuwa ameongozana na marehemu Mohamed
Mhina (35) mkazi wa eneo hilo alijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali
katika mkono wake wa kulia.
Kamanda
Kashai alisema kuwa tukio hilo lilifanywa na watu wawili wa jamii ya wafugaji
na walikuwa wamevaa nguo za kimasai na inasadikiwa kuwa ni wakazi wa kijiji cha
Lembapuri wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Alisema
kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kugombania malisho ambapo watuhumiwa walilisha
mifugo yao kwenye shamba la mabua yaliyokuwa shambani baada ya mavuno katika
eneo hilo la mafisa.
Hata
hiyo alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya
Kilindi kwa ajili ya uchunguzi wakati jeshi hilo linaendelea na msako mkali
kuwatafuta wahalifu waliohusika kwenye tukio hilo.
EmoticonEmoticon