Mhariri
Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya, akikabidhi cheti kwa
mwanafunzi Ahmed Adamu katika mahafali ya tano ya wahitimu wa Kidato cha
nne katika Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyopo Kijitonyama
jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mwenyekiti wa walimu wa maarifa ya
Uislamu Dar es Salaam, Suleiman Gombe.
Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya akizungumza katika mahafali hayo.
………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kutambua wajibu kwa kuhakikisha wanawekeza kwenye elimu kwa watoto wao.
Wito huo ulitolewa Dar es Salam na
Mhariri Msanifu wa gazeti la MTANZANIA, Khamis Mkotya alipokuwa
akizungumza katika mahafali ya tano ya Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu
wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete.
Mkotya ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika mahafali hayo ambapo alisema ni lazima jamii ikubali kuondokana
na kulalamika na badala yake iandae mazingira mazuri ya watoto wao
kuhakikisha wanasoma kwa bidii.
“Bado siku chache wanafunzi wa
kidato cha nne nchini, mtafanya mitihani ya kuhitimu lakini tambueni
kumaliza elimu hii kwa ngazi yetu ni chachu ya kutafuta zaidi ya elimu.
“Na mkiwa hamtafanya hivi mtakuwa
mmekwenda ninyume na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) ambaye
amatutaka tutafute elimu hadi uchina. Na hata leo ukimaliza mtihani wa
kidato cha nne na kuona umemaliza tambueni elimu mlionayo sasa ni sawa
na elimu ya msingi,” alisema Mkotya.
Alisema ili maendeleo chanya
yaweze kupatikana nchini ni lazima jamii ijiandae vema kuyapokea kwa
kuwa na mkakati hasa kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii kwenye masomo
yao.
EmoticonEmoticon